Menu
 

Baraza la vyama vya soka Afrika mashariki na kati CECAFA limetoa kauli ya kupinga taarifa iliyotolewa bungeni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernand Membe mwishoni mwa juma lililopita juu ya usalama wa timu zinazotarajiwa kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Kagame ambazo ni Dar es salaam Young Africans, Simba pamoja na Falcon kutoka visiwani Zanzibar.

Katibu mkuu wa CECAFA Nicolas Musonye amesema kauli ya waziri Membe haina ukweli wowote na imegubikwa na masuala ya kisiasa hivyoa mewataka viongozi wa timu za Tanzania kutokua na wasi wasi na suala la usalama wa vikosi vyao vitakapokua mjini Darfur.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernand Membe alizungumzia hali ya kiusalama ya mji wa Darfur baada ya kuulizwa uhakika wa kiusalama wa timu za Tanzania wakati bunge lililpokua likipitisha bajeti ya wizara hiyo.

Michuano ya Kagame imepangwa kufanyika katika miji ya Darfur ya Kaskazini pamoja na Cordofan ya Kusini, Kuanzia Juni 18 mpaka Julai 2 mwaka huu ambapo kutakuwa na makundi matatu ambapo Kundi A lina timu za Merreikh-Elfasher ya Sudan, APR ya Rwanda, Simba ya Tanzania na Elman ya Somalia.

Kundi B lina timu za Al-Hilal-Kaduugle ya Sudan, Tusker ya Kenya, Al Nasir ya Sudan Kusini, Falcon ya Zanzibar na Al Ahly Shandi ya sudan huku kundi C likiwa na timu za Yanga ya Tanzania, Express ya Uganda, Ports ya Djibouti na Vital O ya Burundi.

Post a Comment

 
Top