Menu
 

Baadhi ya ndugu na marafiki wa Mtanzania aliyehukumiwa kifungo cha miaka nane nchini Angola baada ya kupatikana na dawa za kulevya alizokua akizisafirisha kwenda Afrika Kusini, wamepaza sauti kuomba msaada wa Serikali ili ndugu yao aje kufungiwa gerezani Tanzania.

Khaleed Bin Abad amesema huyu Mtanzania aliondoka South Afrika na kwenda kufata dawa za kulevya Brazil na akafanikiwa kuchukua ila wakati anarudi Afrika Kusini kwenye kubadilisha ndege Angola alikamatwa na kukutwa na dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita.

Kwa kipindi chote hicho huyu jamaa amekua akishikiliwa Angola bila kujua hatma yake na hata kushindwa kukutana na balozi wa Tanzania Angola lakini wiki mbili zilizopita ndio amehukumiwa kifungo cha miaka 8.

Ombi lililoambatana na ndugu hawa kupaza sauti, ni kuiomba serikali kusaidia mtu huyu kukutana na balozi wa huko ili utaratibu wa kuja kufungwa Tanzania ujulikane.

Mara nyingi Mtanzania huyu amekua akituma msg kwa kutumia simu za watu wengine aliokutana nao gerezani.

Post a Comment

 
Top