Menu
 


1. MWAKA 2006 nikiwa tanga nilitoroka shule
asubuhi nikamfukuzia Mtangazaji wa Clouds Fm ya
jiji Dar es Salaam, Hamis Mandi 'B-12' aliyekuja
Tanga nadhani kwenye show ya Park Lane!! am
not sure, nikamkuta ameshapanda basi na
anataka kuondoka ikanibidi nikadandia basi na mimi na kuanza kumtafuta miongoni mwa abiria,
kipindi hiyo hata simjui kwa sura nikasema
atakayekuwa brazameni tu humu ndani ndio
yeye, huku basi linaenda niligonganishana naye
macho akasmile nami nikasmile, nikamfata
nikamkabidhi cd ikiwa na nyimbo zangu 2 nilizirekodi kwa marehemu Mr. Ebbo zamani sana
Motika Record!!! MUNGU AMREHEMU!! "Braza
ngoma zangu hizi samahani naomba kanipigie
zipo poa sana na Tanga zimekubalika mno
samahani sana kanipigie", akawa ananisisitiza poa

zimefika kama kali zitapigwa, we shuka uwahi shule maana basi linazidi kwenda, nikashukia
majani mapana kule kutokea standi!!!


Hazikupigwa zile ngoma na msoto ukaendelea
kama kawa!! nadhani hazikuwa na kiwango bora
au mimi sikuwa mkali!!!! 2. MWAKA 2007 nilirecord nyimbo yangu ya
kwanza SALUTE kwa producer Abbuy wa Tanga,
Studio za GOMBA RECORD, sasa wakati naipeleka
Dar kwenye vituo vya redio nikakutana tena na
B-12 akaniunganisha kwa Dj Nelly ambae alikuwa
mjengoni kipindi hicho kama mmoja wa watu waliokuwa wanafanya kitengo cha muziki pale
Clouds Fm. Basi nikafika mjengoni kitega uchumi
pale mchana mapema nimeambiwa nifike saa
kumi mimi nimefika saa tisa, adabu za kale mbele
hapo, kufika nje nikamwambia mlinzi nataka
kumuona B-12 nina ahadi naye, daah nilipewa mkwara, nikaambiwa nikamngoje chini. Sijakaa
sawa mara bwana Matonya naona anapita pale na
anaingia ndani bila bugudha kwa mlinzi, kidogo
tena nikamuona A.Y naye akapita bila kuulizwa
lolote, daaah moyoni nikawa natukana
kimoyomoyo. Baadae B-12 akatoka akanipeleka hadi kwa Dj Nelly, ilikuwa kama oyaa Dj Nelly
msikilize huyo mdogo wangu...dah jamaa akawa
kama hasikii vile apo nimesimama na kacd kangu
pembeni nashangaa tu kumbe huyu ndiyo Gadner
na huyu ndiyo P.J okey hapo Jahazi ndiyo linataka
kuanza. Dj Nelly akaanza kusema 'oya sema shida yako?'
nikajibu aaah braza mimi naitwa Ro....
akanikatisha haraka na kuniambia nina dakika 2
tu za kuongea naye, kisha akachukua CD
akaiweka kwenye machine vile inaanza tu
akaisimamisha hakuicheza tena, na hapo yani kaisikiliza nyimbo ndani ya sekunde 15 au 20
akaitoa CD na kunijibu hamna kitu Production
mbovu na huwezi kuchana!!! kisha akamgeukia
Gadna na kuendelea na hadithia zao, mimi
nikamuuliza sasa braza nishauri nifanyaje? Oyaa
dogo tuna maongezi hapa huoni!!? hatuwezi kupiga nyimbo kama hiyo akanijibu kwa ukali...
dah nikakosa pozi nikaanza kusepa, huku
moyoni najisemea, aah wewe Gadna si ni Mtanga
mwenzangu wewe hata hutii neno kaka?.
Nikamfata B-12 wangu maana ndiyo alikuwa
kimbilio langu mjini hapa, naye hakuwa na jinsi wal anamna ya kufanya maana hawezi kupiga
nyimbo kama kitengo cha muziki hakujaruhusu,
akanishauri nikairudie nyimbo ile kwa Dunga...
kipindi hiyo Dunga alikuwa ndiyo gumzo. Hivyo
nikatoka pale nikaipeleka ngoma ile ile East Africa
Radio nikaiandikisha na nikasepa hapo nauli inaelekea kuliwa, babaako nikalirudisha kunani
Tanga moja. Aaah! East Africa Radio bana wakanipigia simu na
kusema nyimbo yako tunaitambulisha leo na
wana segment inaitwa ipotezewe au iendelee
kuwepo kitu kama hicho... basi nikiwa Tanga
nikatega sikio kwenye satelite kusikiza baadae
wakaipiga na ikapata kura 338 zikisema iendelee kuwepo na kura 34 zikisema ipotezewe
nakumbuka hadi leo hiyo!!! basi nyimbo yangu
ikapita na ikawa inapigwa pigwa east East Africa
Radio. Wakati huo huo samahani kabla sijaenda
Tanga, nikiwa Dar nilikutana na Jaffarai alikuwa ni
rafiki wa karibu wa braza yangu, braza akanitambulisha "Huyu mdogo wangu anaitwa
Ebra au ROMA anarap na kaleta nyimbo yake"...
hapo natamani jamaa aseme tuisikize... (si unajua
zile ukiwa unajiamini na nyimbo ni nzuri) basi
tukamshawishi aisikize, basi tukaenda kwenye
gari na akaiweka. Uwiiiiiiii! Jafarai akaanza "Aaah mbona anachana kama mwana FA? aaah! hana
style yake huyu babu, tafuta style yako mzee,
game gumu mzee, njoo kivyako man", sasa
nikawa najiuliza nachana vipi kama Mwana FA?
mh! nikaona ananikata tu nikamchana braza
tuondoke bwana naona navurugwa tu. Tukaaga tukaondoka kinyonge!! 3. MWAKA 2008 nimeshajichanga nipo safi ndiyo
nakuja Dar rasmi sasa kurekodi TANZANIA hapo
nimeshaongea na Nahreal, na pia nakuja kuirudia
ile ngoma iliyokataliwa radio nakuja kuirudia kwa
Dunga. Ndipo hapo tukiwa na braza mitaa ya
mikocheni nadhani. Ndio tunakutana na Fid Q, Jafarrai na Mussa Hussein wa uswazi yule, tukafika
na kaka hadi pale tukasalimia pale ila si unajua
kisanii mara nyingi ukimsalimia mtu ni kama
anakuwa anakukataa hivi anaitikia short short
ndivyo ilivyokuwa. Sasa kaka akaanza kuongea
na Jafarai mambo yao tu aaah! katikati ndiyo wakachomekea kaka akamwambia Jaffarai "Aah!
tunaenda 41 Record kwa Dunga nampeleka
mdogo wangu huyu si unamkubuka"?? Jafarai
akajibu aaah! huyu si yule wa kipindi kileee? hapo
ujue mwaka umeshapita hapo, kaka akamjibu
ndiyo huyu sasa amekuja kuirudia ile ngoma huku kwa Dunga!! Jafarai akasema aaah amebadilika? au bado
anachana vile vile? dogo badilika aisee! game
gumu sana dogo kwa style ile unapoteza hela tu
huwezi kutoka, sasa akaanza kunivuruga tena ila
moyoni nikawa nasema " Mbona Fid Q haununui
huu ugomvi? yani kwanini haulizi lolote daah! hapo Fid Q kajikausha hata hatusikilizi yani yeye
busy wanaongea na Mussa tu, mimi nikawa
natamani kaka aseme kitu tu. Hatimaye Fid Q
akaingilia "Oya kwani vipi babu? mbona kama
unamnyea sana jamaa"? akamuuliza Jafarai?
Jafarai akajibu "Aah! huyu dogo alikuja huku kama mwaka umepita hivi, akaniletea nyimbo
yake, ila ni ya kiwaki!! sasa kaenda kujipanga na
sasa karudi rasmi... Fid akasema niaje babu?
unaimba au unarap? nikamwambia narap!!
akasema ok 1,2,3 twendee... mamamammama
ndiyo nilichokisubiri kwa muda mrefu hiki. Nikaanza kuchana nyimbo ile iliyokataliwa radioni
na iliyopingwa na Jafarai... sasa kadri ninavyozidi
kuchana naona jinsi bwana Kubanda anavyozidi
kunogewa, namimi naongeza misifa hapo
nachana tuu kwa hisia. Ikawa poa sana kwake na
akakubali hadi kuamka kwenye kiti na kunipongeza kuwa am good, lakini moynoi
nikawa nataka nimchanie TANZANIA maana ndiyo
nimekuja kuirekodi na ndiyo nina mzuka nayo na
ndiyo naiona ni nyimbo kali, yani zile za (kama
kadata nahii tu je Tanzania nikichana itakuwaje)?
sasa nikamwambia ngoja nikuchanie nyingine... akakataa akasema aaah! mimi sitaki nyingine,
nichanie hii hii iliyokataliwa. Sasa nikapita nayo tena. Sasa ujuee na nyimbo
hiyo ninayochana hapa ndiyo baadhi ya mashairi
yake yamepita tena kwenye MATHEMATICS na
MECHI ZA UGENINI... niliyarudia kwa vile sikutaka
yapotee bure vitu kama "Ndoto zangu kitambo
zilikuwa nije kuwa padre, zikayeyuka nilipopuliziwa moshi wa weed etc. Basi Fid Q
alikubali sana na hapo ndipo akasema una IQ
sana bab...ndio chanzo cha ule mstari wa kusema


"Nawazidi kwa IQ shahidi Fareed Kubanda"!
ambapo tazama sasa nimeuimba kwenye ngoma
ya 4 toka niambiwe hivyo na yeye. Basi alikubali sana na akasema ni bora nikarudie kwa Macko
Chali na akawa anampigia simu sema Marco
hakupatikana akaniachia namba yake, sasa
Jafarai na yeye alipoona Fid Q anakubali akawa na
yeye anasema aah! dogo sasa amebadilika sasa
hahaha! moyoni nikawa na furaha sana unajua inavyokuwa unakubaliwa na watu kama hawa
kwa kipindi hicho u konw it!! nikaondoka na
kaka tukawaacha majamaa, nikaendelea na hasso
za kurekodi kwa Dunga na Nahreal!!! HIZO NI BAADHI ZA MICHONGO ILIYOHAPPEN
KABLA HAIJATOKA WALA KUREKODIWA NGOMA YA
KWANZA YANGU ILIYONITAMBULISHA "tanzania" 4.
BASI YAPO MENGI SANA YANAJAA KITABU
NADHANI NA MENGI NI YA KUSISIMUA. NATAMANI
NIPATE INTERVIEW TENA YA TV HARAFU NIHADITHIE KWA SAA MOJA NA ZAIDI YOTE HAYA.
SEMA YOTE HAYA UTAYAPATA KWENYE
"DOCUMENTARY YA ROMA 2030" KUANZIA
NAZALIWA HADI HAPA NILIPO SASA. (UZURI NI
KUWA KUNA BAADHI YALIREKODIWA SO ITAKUWA
IPO REAL SANA). TUENDELEE KUNGOJA!!! NAJUA MNAENJOY NIKIFUNGUKA HIVI YAPO MENGI KAMA;
1. Mimi kukutana na kala na kugonganisha
mawazo ya wimbo wa Tanzania na wa kwake wa
wimbo wa Taifa. 2. Nakaaya kunizingua kwenye
kumshirikisha katika ngoma yangu ya Tanzania,
ila badae alinitafuta na kuniomba kolabo baada ya kutoka Mathematics. 3. Wasanii wakubwa
kunikatalia kwenye kolabo zangu kama Mr.
President na Tanzania, ndiyo maana nasimama
bila kumshirikisha mtu kiivyo. 4. Nikki wa Pili
alisababisha nikarekodi mechi za ugenini though
yeye hajui hili. 5. Nilivyoingia kwa Duke M. LAB na kurekodi Mr. President lakini haikutoka, na mimi
nikahamia Tongwe na kuanza kurekodi upya
hadi leo nipo Tongwe. 6. Nilihit sana na Tanzania lakini Jay MO aliwahi
kuniambia hanifahamu... ila siku zikaenda akaja
akanifahamu na tukafanya naye MVUA NA JUA
REMIX kwa majani. 7. Kwanini wadau wengi
wakati natoka na Tanzania hadi Mr. President
walinambia THAT IS HIP HOP!!! safi kaza mwana harafu leo inatoka hit kama Mathematics
wanasema sifanyi hip hop!! napayuka!!
naropoka!! napiga makelele!! sina stye!! na mengi
tu hadi kusema tuzo sikustahili.... duuuh! HATARI
AISEE! 8... NYIMBO YANGU YA TANZANIA
ILIVYOKATALIWA NA RADIO STATIONS NYINGI, ADAM MCHOMVU ALIKUWA MBISHI SANA THANKS
GOD AKAIPITISHA NA RADIO ZA MIKOANI
ZIKASSUPORT MNO!! ..9.......10..... Nawapenda sana
watu wangu kuna vita kubwa sana dhidi yetu basi
katika sala zenu msinisahau kuniombea niwe na
afya njema na maisha yenye heri na baraka na marefu mimi na familia yangu na Tongwe wote na
ndugu jama na marafiki
wote!!!.

Post a Comment

 
Top