Menu
 

Jamaa alikuwa anampenda kweli Kidoti, akikuta gazeti lenye picha ya binti huyo lazima alinunue, lakini akawa hana njia ya kuwasiliana na Kidoti kumueleza yaliyomo moyoni mwake. 

 Siku moja akabahatika, rafiki yake mmoja akampa namba ya simu ya Kidoti, hakuamini bahati hii, akarudi nyumbani anatetemeka anapanga maneno mazuri ya kuandika katika mesej kupeleka kwa Binti Kidoti.

 Hatimae usiku akiwa kitandani kwake akaweza kutunga maneno matamu ya kumtoa nyoka pangoni, akiwa na uhakika kuwa Kidoti hawezi kukwepa kupata hisia akatuma mesej ile.

Dakika chache baadae, simu ikatoa mlio kuonyesha kuwa kuna mesej imeingia, jamaa jasho likamtoka kwa furaha akiwaza aina ya jibu ambalo litakuwa limetoka kwa Kidoti. Akaona ili afaidi heri ajibane asome mesej ile asubuhi baada ya chai.

 Asubuhi akawahi kuamka na kuoga vizuri, akanywa chai kisha akachukua simu na kufungua meseji toka kwa sabuni yake ya roho. Akakuta mesej ikisema,' Salio lako halitoshi kutuma ujumbe huu tafadhali ongeza salio' 

Post a Comment

 
Top