Menu
 

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza Roy Hodgson amesema hakufurahishwa na matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili yaliyopatikana baada ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa fainali za kombe la mabara pamoja na zile za dunia timu ya taifa ya Brazil.


Roy Hodgson amesema hakuona sababu kwa kikosi chake kukubali matokeo hayo kutokana na uwezo mkubwa waliouonyesha dhidi ya timu ya taifa ya Brazil ambayo ilikua nyumbani ikicheza kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Maracana tangu ulipoanza klufanyiwa marekebuisho kwa ajili ta fainali za kombe la dunia za mwaka 2014.


Hodgson amesema licha ya timu ya taifa ya Brazil kuonyesha uwezo wa kucheza kwa kujiamini wakati wote, bado kikosi cha Uingere3za kilikua na nafasi nyingine ya kuchomoza na ushindi.Katika mchezo huo Timu ya taifa ya Brazil ilikua ya kwanza kulisabahi lango la timu ya taifa ya Uingereza kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya Fluminense Frederico Chaves Guedes *Fred* kabla ya vijana wa samba watatu hawasawazisha kupitia kwa winga wa klabu ya Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain na kisha Wayne Mar Rooney kufunga bao la pili ambapo hata hivyo lilisawazishwa na  José Paulo Bezerra Maciel Júnior, *Paulinho*.


Huu unakua mchezo wa pili kwa timu ya taifa ya Uingereza kuambulia matokeo ya sare ambapo kama itakumbukwa vyema kikosi hicho cha roy Hodgson kilishindwa kutamba mbele ya jamuhuri ya Ireland kati kati ya juma lililopita.

Post a Comment

 
Top