Menu
 

 Pichani katikati mrembo huyo baada ya kuvishwa taji hilo.
Aliyekuwa mshindi katika shindano la kumtafuta mrembo wa wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, Redd’s Miss Nyamagana 2013 Diana Amimo amevuliwa taji hilo baada ya kubainika kudanganya umri wake pamoja na uraia, kasoro zilizompunguzia sifa za kuvaa taji hilo.

 Mratibu wa shindano hilo lililofanyika (May 11) jijini Mwanza, bwana Mukhsin Mambo wa Stoppers Entertainment, ameeleza kuwa baada ya kugundua mapungufu hayo kwa Diana, kamati ilikaa (June 6) na kuamua kumvua taji hilo na kumvisha aliyekuwa mshindi wa pili Rosemary Peter ambaye sasa ndio Redd’s Miss Nyamagana 2013. 

Mr. Mambo amesema udanganyifu huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza wiki moja baada ya shindano hilo, baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo na kubaini kuwa Diana ni raia wa Kenya na ana umri wa miaka 17. 

Kwa Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24

Post a Comment

 
Top