Menu
 

Hatimae meneja kutoka nchini Ureno, José Mário dos Santos Félix Mourinho amekamilisha mpango wa kurejea ndani ya klabu ya Chelsea akitokea kwenye klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ambayo ameitumikia kwa muda wa miaka mitatu. Jose Mourinho amerejea kwenye klabu ya Chelsea kwa lengo la kuchukua pahala palipoachwa wazi na meneja Rafael Benitez ambae aliingia mkataba wa kukinoa kikosi cha klabu hiyo wa muda wa miezi zita tangu mwishoni mwa mwaka jana.Mtendaji mkuu wa klabu ya Chelsea Ron Gourlay amethibitisha taarifa za kurejea kwa meneja huyo ambae amekubalia kusaini mkataba wa miaka minne ambao utamuweka Stamford Bridge hadi mwaka 2017.Kuirejea kwa meneja huyo kumezua mazungumzo mengi katika vyombo vya habari karibu ulimwengu mzima ambapo wengi wanahoji wakati wa Jose mourinho kukubali kukinoa kikosi cha Chelsea kwa mara nyingine tena kama ni sahihi.Mchambuzi wa taarifa za michezo wa kituo cha televisheni cha CNN cha huko nchini Marekani Alex Thomas amesema anaamini kurejea kwa meneja huyo mwenye umri wa miaka 50 ndani ya klabu ya Chelsea ni muda sahihi kutokanana na mafanikio aliyoyapata kabla na baada yta kuondoka kwake klabuni hapo mwaka 2007.Jose Mourinho anarejea Chelsea huku akikuta mafanikio makubwa yaliyofikiwa bila ya yeye kuwepo ambapo tangu alipoondoka mwezi September mwaka 2007 The Blues wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya pamoja na ubingwa wa Europa League na pia wamefanikiwa kucheza michuano ya ligi ya mabingwa duniani na kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

 
Top