Menu
 

Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hospitali ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

Aminiel Aligaesha ambae ni Afisa Uhusiano wa hospitali ya Taifa Muhimbili amethibitisha kwamba msanii Langa amefariki dunia June 13 2013 saa kumi na moja jioni baada ya kufikishwa hospitalini hapo toka juzi jioni ambapo kutokana na sababu za kimaadili kwenye tiba, Muhimbili hospitali hawawezi kusema rapper huyu alikua anaumwa nini bali ndugu ndio wenye mamlaka ya kufanya hivyo.

Kwenye maelezo aliyoyatoa Aminiel amesema Marehemu Langa alipokelewa kwenye idara ya wagonjwa wa magonjwa ya dharura usiku wa kuamkia jana na kupatiwa huduma ambapo leo June 13 2013 ndio alihamishiwa kwenye chumba cha wagonjwa Mahututi na baadae kufariki dunia.


NA HII NI KAULI YA Msanii mwenzake SHAA baada ya kupata taarifa ya kifo chake.
Mlimfahamu kwa kipaji chake...Lyrically And Naturally Gifted African...ila vilevile alikuwa a brother,mdogo mtu,an uncle,a son...a son....but cha zaidi,alikuwa binadamu kama mimi na wewe...umenitangulia tu...i will see u again and make my peace...untill then pumzika kwa amani,God bless u na ur family.

Post a Comment

 
Top