Menu
 

.
.
Kutokana na viongozi wakuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuzuiwa kuingia ndani ya bunge wakiwa wamevaa sare za chama, wabunge wa Chadema wamesusia kuhudhuria kikao cha kupitisha bajeti ya serikali 2013/14 jioni hii ya June 24 2013.
Huo uamuzi umetangazwa na mnadhimu mkuu wa kambi hiyo Tundu Lissu ambapo  amesema ni kinyume na kanuni ya bunge inayozungumzia mavazi rasmi ya wabunge wanaume.
Arusha mabomu june 18 2013
 
Namkariri Tundu Lissu akisema “Tumeona hatuwezi kushiriki katika shughuli ya bunge ya leo, tunakwenda kushiriki nini? kufanya uamuzi wa aina gani? wakati hatujashiriki kwenye mjadala kwenye mjadala kwa sababu ambazo tumezieleza, hatuwezi tukaingia bungeni kupiga kura kuamua kitu ambacho hatukukijadili, tumezuiwa kukijadili, tukio la bomu la Olasiti Arusha Mh Spika aliongoza ujumbe wa Wabunge karibu 30 kwenda kuwapa pole na kuangalia eneo la tukio, this time watu wameumizwa, watu wamekufa, bunge halijaahirisha shughuli halitoa mchango hata senti kumi na hakuna hata wazo la kwenda kuwaona walioumia na waliofiwa”
Kwenye sentensi nyingine, Tundu Lissu ameonyesha kushangazwa na bunge kuendelea na majadiliano ya uchumi wa Taifa 2012 na mpango wa maendelea ya Taifa 2013/2014 wakati kukiwa na tukio la mauaji lililotokea Arusha ambapo watu watatu walifariki dunia.
Hata hivyo wakati Chadema wakisusia kikao cha bunge, wabunge wengine walikua wanatarajia kuipitisha bajeti hiyo ya Serikali ya 2013/14 iliyotenga zaidi ya Trillioni 18.2 (kwa hisani ya Millardayo.com)

Post a Comment

 
Top