Menu
 

AMRI KIEMBA
Chama cha wachezaji wa soka nchini SPUTANZA kwa udhamini wa Peps mwishoni mwa juma lililopita kilifanikisha azma ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji pamoja na makocha waliofanya vyema katika msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa mwaka 2012-13.

Hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam, ilishuhudia wadau wachache wakijitokeza, hali ambayo imepokelewa tofauti na uongozi wa SPUTANZA kwa kukiri japo ni mwanzo wameona walifanya makosa katika utaratibu wa kuitangaza siku hiyo.

Katibu mkuu wa SPUTANZA Said George amesema watayafanyia kazi mapungufu hao kwa kiasi kikubwa ili hafla ya utoaji wa tuzo kwa wachezaji na makocha watakaofanya vizuri msimu ujao iweze kufana.

Katika hafla hiyo inayojulikana kama SPUTANZA FOOTBALL AWARDS wachezaji watatu pamoja na kocha mmoja walizawadiwa baada ya kujizolea kura nyingi zilizopigwa na jopo la makocha.
Tujikumbushie namna ambavyo washindi walivyo tangazwa
1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu - Amri Kiemba (Simba)
Amewashinda
Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu (Yanga),
Kipre Tchetche (Azam),Paul Nonga (Jkt Oljoro)

2. Kocha Bora wa Mwaka - Mecky Maxime (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Boniface Mkwasa (Ruvu shooting),Abdallah Kibaden (Kagera Sugar) Jumanne Charles (Prisons)

3. Mchezaji Bora Chipukizi - Salum Abubakar "Sure Boy" (Azam)
Amewashinda
Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Issa Rashid (Mtibwa)
Shomari Kapombe (Simba) Twaha Shekue (Coastal Union)

4. Golikipa Bora - Hussein Sharif "Casilas" (Mtibwa Sugar)
Amewashinda
Juma Kaseja (Simba), Mwadin Ally (Azam).

Zawadi ya mchezaji bora wa msimu uliopita imekwenda kwa ya kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa Taifa Stars pamoja na klabu ya Simba Amri Kiemba.

Hata hivyo cha kushangaza tuzo ya mchezaji huyo ilipokelewa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu ay Dar es salaam Young Africans Mohammed Binda ambae akatoa siri ya kumuwasilisha Amri kiemba.

Post a Comment

 
Top