Menu
 

Mkuu wa wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa Mbeya  akihutubia mamia ya wakazi wa mkoa wa Mbeya waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto(GBV) utakaoendeshwa kwa majaribio kwa muda wa miezi 18 kwenye baadhi ya maeneo ya wilaya sita zilizopo mkoani Mbeya
Mkurugenzi wa shirika la Walter Reed kanda ya nyanda za juu kusini Cmeron Garrette akielezea umuhimu wa mradi huo kwa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo 
Meneja mradi  Walter Reed Hijja Wazee akisoma risala mbele ya mgeni rasmi

Shirika la Walter Reed Tanzania limekabidhi vifaa vya kimaabara pamoja na vitanda maalum kwa ajili ya akina mama wakati wa kujifungua vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 300.
Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi mkazi wa Walter Reed, Kanda ya Nyanda za Juu kusini Cameron Carete kwa Kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya Deodatus Kinawiro, amesema msaada huo umetolewa ili kuboresha huduma ya afya katika Hospitali za mkoa wa Mbeya.
Akihutubia maelfu ya wakazi wa mkoa huo Juni 20 mwaka huu katika uzinduzi huo Kaimu mkuu wa mkoa wa Mbeya Deodatus Kinawiro, ametoa pongezi kwa shirika hilo kwa msaada walioutoa.
Naye Meneja wa mradi Kanda ya Nyanda za Juu kusini Bi Hija Wazee amesema mkoa wa Mbeya umechaguliwa kusimamia mradi huo wa kupinga ukatili wa kijinsia na watoto(GBV) utakaoendeshwa kwa majaribio kwa muda wa miezi 18 kwenye baadhi ya maeneo ya wilaya sita zilizopo mkoani Mbeya.
Awali akisoma ripoti ya dawai la ujinsia mkuu wa dawati hilo kutoka Jeshi la Polisi Bi Mery Gumbo, amesema hivi sasa jamii imekuwa na uelewa mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita

Post a Comment

 
Top