Menu
 Baada ya ya wadhamini wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, kuonyesha bado wana imani na mpango wa kocha mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Kim Poulsen, shiriklisho la soka nchini TFF nalo limeonyesha kuwa na matumaini makubwa na kocha huyo kutoka nchini Denmark.Katibu mkuu wa TFF Angetille Osiah amesema licha ya timu ya taifa ya Tanzania taifa stars kushindwa kufikia malengo ya kucheza fainali za mataifa bingwa ya Afrika CHAN baada ya kufungwa na timu ya taifa ya Uganda, bado wanaendelea kuamini malengo ya kocha huyo ya kucheza fainali za Afrika za mwaka 2015 yataweza kufikiwa.Katika hatua nyingine Angetille Osiah amesema wanatambua matokeo ya kufungwa na timu ya taifa ya Uganda yamemsikitisha kila mdaui wa soka nchini ambe alikua na matumaini makubwa na timu ya taifa katika fainali za CHAN mwaka 2014.Osiah amesema mazingira ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita yalifanana na mazingira ya michezo mingine ambayo Taifa Stars walipoteza wakati wa fainali za kombe la dunia hivyo amekiri kuwepo kwa uzembe ambao ana hakika utafanyiwa mrekebisho la kocha Kim Poulsen.

Post a Comment

 
Top