Menu
 


Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kesho kinatarajiwa kuwasilisha maoni ya katiba mpya kwa tume ya mabadiliko ya katiba baada ya kukamilisha mzunguko wa kukusanya maoni kwa baadhi ya wananchi nchi nzima.Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbroad Slaa amesema jumla ya watu milioni 3,462,805 wametoa maoni yao kwa chama hicho kwa njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya hadhara, simu na barua pepe.Akiongea na wandishi wa habari jijini Dar es salaam, pamoja na mambo mengine Dk Slaa ametaja jumla ya mapendekezo 11 ambayo hayapo katika rasimu ya katiba iliyotolewa na tume ya Jaji Joseph Warioba ambayo wangependa yaingizwe katika katiba.
Mapendekezo mengine ni haki ya kupatiwa malipo ya uzeeni pamoja na msaada wa hifadhi ya jamii kwa gharama ya serikali wakati wa uzee kwa watu wote, haki ya kupata msaada wa matibabu na kutaka siku ya kupiga kura isiwe ni siku ya kuabudu ya imani ya dini yoyote ile.Mambo mengine ni pamoja na rais kushitakiwa endapo atabainika na kosa lolote la jinai chini yasheria au chini ya mkataba wowote wa kimataifa ambo jamhuri ya muungano ni mwanachama ambao unakataza kinga dhidi ya mashtaka ya raisi.

Post a Comment

 
Top