Menu
 


Hatimae shirikisho la soka nchini TFF limeingia mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Azam Media kwa ajili ya kuonyesha michezo ya ligi kuu ya soka Tanzania bara kuanzia msimu wa mwaka 2013-14.


Katika hafla hiyo ya utiliaji saini, TFF wamewasilishwa na makamu wa kwanza wa raisi Athuman Nyamlani, Katibu mkuu Angetille Osiah pamoja na mwanasheria wa shirikisho hilo Alex Mgongolwa.


Kwa upande wa Azam Media mkurugenzi wa kampuni hiyo Rhiys Morington alikuwa muwakilishi mkuu ambapo alikamilisha mipango ya utiliwaji wa saini katikaa mkataba wa uonyeshaji wa ligi hiyo.


 Makamu wa kwanza wa raisi wa TFF Athumani Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi ndani na nje ya nchi.


Hata hivyo Nyamlani akazungumzia sakata la mabingwa wa soka tanzani bara Dar es salaam Young Africans ambao wamekua wakidai haki ya kutaka kulipwa zaidi ya klabu nyingine 13 za ligi kuu.


Kwa upande wa mkurugenzi mtendaji wake, Rhy Torrington amesema wamefurahishwa na zoezi hilo kukamilika na sasa wanahakika kila mtanzania atakua na haki ya kuifuatilia ligi kuu ya soka tanzani bara ambayo imekua ikikua siku hadi siku.


Azam TV ambayo ni moja ya chaneli za Azam Media itakuwa na chaneli 50 na juma lijalo kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wake, Rhy Torrington itaanza kurushwa kwa majaribio.

Hata hivyo, Torrington amesema hatakubali kuona Azam TV inaanza kuonekana kama hataridhika na kiwango chake cha matangazo.

Post a Comment

 
Top