Menu
 

 
Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe akizungumza na waandishi wa Habari nanenane 

  Mkurugenzi wa Bahari Zoo anaeleta wanyama hai   Willy Kusaga Nanenane akizungumza na waandishi wa Habari
 Mkurugenzi wa kampuni ya MLM International Vision (T) Limited William Mkandawile akifafanua Jambo
 Fisi akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Simba Jike akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Simba Dume akiwa tayari katika viwanja vya maonesho
 Waandishi wakipata ufafanuzi wa maonesho ya Nanenane  mwaka huu 2013 katika mkutano uliofanyika katika ofisi za TASO Mbeya.

***********
BAADA ya kiu ya Muda mrefu kwa Wakazi wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini ya kutokuwaona Wanyama hai kwa zaidi ya miaka 30, hatimaye Maonesho ya Nanenane Mwaka huu yatakayofanyika Kikanda Mkoani Mbeya Wameletwa.

Wanyama hao wanaoletwa kwa Udhamini wa Kampuni ya Pepsi na MLM International Vision (T) Ltd kutoka katika Kampuni inayohusika na Wanyama hai ya Bahari Zoo kutoka Jijini Dar Es Salaam itatoa fursa kwa Wakazi wa Kanda hii kujionea kwa ukaribu na kumaliza kiu ya Muda mrefu.

Akizungumza katika mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Leo katika Viwanja vya John Mwakangale Uyole Jijini Mbeya, Mkurugenzi wa Bahari Zoo Willy Kusaga amesema kwa utafiti wake amebaini kuwa mara ya mwisho wanyama kama Simba, Chui, Chatu, Mbega, Fisi na wengine walikuja Mbeya Mwaka 1977.

Amesema yeye binafsi anajisikia fahari kuona Wakazi wa Mbeya walivyoitikia ujio wa Wanyama hao na kwamba utalii wa Ndani utatangazwa vilivyo na kuhamasisha Wananchi kuanza kupenda kutembelea vivutio vilivyojirani na makazi yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (TASO) Kanda ya Mbeya, Noel Nkoswe alisema maandalizi ya Nanenane Mwaka huu ni makubwa kutokana na watu kuham,asika na waoneshaji kuongezeka tofauti na maonesho ya nyuma.

Amesema hamasa kubwa imetokana na kiu ya kuwaona wanyama kutokana na kutokuwepo kwa muda mrefu na wengine kukosa fursa ya kutembelea mbuga za Wanyama zilizozoeleka ikiwa ni sababu za uchumi na umbali.

Ameongeza kuwa sababu nyingine itakayoleta hamasa ya maonesho ya Mwaka huu ni fursa ya kuandaa maonesho ya Kitaifa yaliyohamishiwa Dodoma kwa Mwaka wa Sita Mfululizo hivyo kuwafanya Wananchi kuamini Mwaka huu kufanyika kitaifa Mkoani Mbeya.

Mwenyekiti huyo amesema katika Uzinduzi wa Nanenane Kwa Kanda hii utafanywa na Waziri Wa Uchukuzi, Dr. Harisson Mwakyembe ambapo Siku zitakazofuata kila Mkuu wa Mkoa atapangiwa siku yake kwa ajili ya Mkoa husika kuonesha shughuli za Wakulima wake.


Alizitaja siku hizo kuwa ni Agosti 2, Mwaka huu kufanywa na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya huku Mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, Agosti 3, Mkoa wa Rukwa, Agosti 4 mkoa wa Iringa, Agosti 5 Mkoa wa Njombe, Agosti 6 Mkoa wa Ruvuma na Agosti 7 utakuwa ni Mkoa wa Katavi.
Picha   na Mbeya yetu

Post a Comment

 
Top