Menu
 Kiungo mahiri wa kimataifa wa Brazil, Kaka amebainisha kuwa anataka kuondoka Real Madrid ikiwa imebakia wiki moja kabla ya kipindi cha usajili majira ya kiangazi kumalizika.Kaka mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akipambana kukuza kiwango chake chini ya kocha wa zamani Jose Mourinho na haonekana kuwa katika mipango ya kocha mpya Carlo Ancelotti baada ya kukaa benchi katika mechi mbili za La Liga msimu huu.Bali na hivyo pia ujio wa Gareth Bale kutoka Tottenham Hotspurs nao unaonyesha kumlazimisha nyota huyo kuondoka baada ya kuona atakuwa hana nafasi tena kwenye kikosi hicho.Kaka amesema anadhani wakati wake wa kuondoka umefika na tayari ameshazungumza na Ancelotti pamoja na viongozi juu ya azma yake.Kaka alitua Madrid akitokea AC Milan mwaka 2009 na toka kipindi hicho amecheza mechi 85 pekee baada ya kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara yaliyochangai kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango chake.

Post a Comment

 
Top