Menu
 

Mfuko wa Pensheni wa PPF upo katika mchakato wa kuhuisha viwango vya pensheni vinavyotolewa kwa wanachama wastaafu kwa kuzingatia gharama za maisha.

Naibu Waziri wa Fedha mheshimiwa Saada Mkuya Salum amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Singida Magharibi mheshimiwa Mohamed Missanga aliyetaka kujua sababu ya PPF kuwakandamiza wastaafu kwa kutokuhuisha viwango vyao vya pensheni.

Mheshimiwa Mkuya amesema si kweli kwamba PPF wanawakandamiza wastaafu bali inategemeana na faida ambayo mfuko inapata.

Amesema  tayari ripoti ya mapendekezo yaliyotolewa ilishaandaliwa  na imepelekwa baraza la mawaziri kwa ajili kuridhiwa.

Mheshimiwa Mkuya amesema ripoti hiyo itaangalia ni namna gani sasa watahuisha viwango vya pensheni kwa mifuko yote ili kuweka uwiano sawa kwa wastaafu ambao wanapata pensheni zao katika mifuko mbalimbali na hiyo itasaidia kuondokana na utofauti.

Katika swali la nyongeza la mbunge wa Kawe mheshimiwa Halima Mdee ametaka kujua  lini serikali itafanya marekebisho ya viwango vya pensheni  kwa wanajeshi waliostaafu ili kuendana na mazingira halisi ya uchumi wa Tanzania.

Akijibu swali hilo mheshimiwa Mkuya amesema kilio hicho cha wastaafu wanajeshi kimekuwa ni kikubwa na hiyo imetokana na marekebisho waliyoyafanya na kuomba kulichukua jambo hilo na kwenda kulifanyia kazi ili wanajeshi hao waweze kupata kile wanachostahili.

Post a Comment

 
Top