Menu
 Mahakama ya jiji la Munich imemfungulia mashitaka rais wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness kwa kosa la ukwepaji kodi baada ya kukamilisha uchunguzi uliodumu kwa miezi kadhaa.


Hoeness ambaye amekuwa kioo cha Bayern kwa miaka kadhaa, alitoa kauli ya kustusha April mwaka huu akidai kuwa aliijulisha mamlaka ya kodi Januari kukagua akaunti yake anayomiliki huko Switzerland.


Msemaji wa mahakama hiyo Andrea Titz amesema mshitakiwa sasa amepewa wiki nne kujibu mashitaka yake ambao amepelekewa mapema jana.


Hoeness ambaye anaweza kukabiliwa na kifungo jela lakini akiwa na mategemeo ya kupata msamaha baada ya kujisalisha mwenyewe, amesema akunti hiyo ya Switzerland iliyokutwa na matatizo haina uhusiano wowote na Bayern.

Post a Comment

 
Top