Menu
 


Ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa wanataaluma nchini serikali inasomesha wanataaluma 80 kila mwaka katika ngazi ya uzamili na uzamivu ndani na nje ya nchi.

Akijibu swali leo bungeni mjini Dodoma Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi mheshimiwa Philipo Mulugo amesema wanataaluma hao wanasomeshwa kupitia ruzuku ya serikali.

Amesema hatua hiyo ni mojawapo ya mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo na kutaja moja ya mikakati mingine kuwa ni kwa serikali kutoa mikopo kwa wanaataluma wanaotaka kujiendeleza.

Pamoja na juhudi hizo amesema bado kuna changamoto ya Vyuo Vikuu binafsi ambavyo kutokana na uchanga wao vinalazimika kuwaajiri wahadhiri kutoka vyuo vikuu vya umma hasa wahadhiri wanaostaafu katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma kwa kuwa kwao ni gharama nafuu kutumia wahadhiri wa ndani kuliko kutoka nje.

Mheshimiwa Mulugo alikuwa akijibu swali la mbunge wa viti maalum mheshimiwa Sara Msafiri aliyetaka kujua sababu ya serikali kutoanzisha utaratibu wa kuajiri kwenye vyuo wataalam kutoka nje ya nchi ili wanafunzi wengi wafaidike na utaalam huo badal ya wananfunzi kwenda kusoma nje wakati gharama ni kubwa.

Post a Comment

 
Top