Menu
 


Slaughter: Syrian activists inspect the bodies of people they say were killed by nerve gas in Damascus

Mamia ya raia wameuawa kufuatia shambulio lililotumia silaha za kemikali viungani mwa Mji Mkuu wa Syria, Damascus. Makundi ya upinzani yanasema makombora yaliyokua na kemikali ya sumu yalilenga eneo la Ghouta usiku wa kuamia Jumatano. Inadaiwa majeshi ya serikali yalikua yakiwashambulia waasi.Hata hivyo Shirika la utangazaji la serikali limetaja taarifa hizo kama upuzi mtupu,na kusema ni kisingizio tu cha kuwachochea wakaguzi wa Umoja wa Mataifa walioko Syria.
Muungano wa upinzani umesema zaidi ya watu 650 waliuawa katika shambulizi hilo.Makundi mengine ya kiraia pia yametangaza vifo vya mamia katika shambulio hilo japo taarifa hizo hazijathibitishwa kirasmi.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague, ametaka utawala wa Syria kukubalia wakaguzi wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo na kusema Uingereza itawasilisha hoja katika Umoja wa Mataifa.

Muungano wa nchi za Kiarabu pia umeunga mkono wakaguzi hao kuingia eneo hilo.Shambulizi hilo ni moja wapo ya operesheni kali ya jeshi la serikali katika maeneo yanayothibitiwa na waasi mjini Damascus.

Maeneo yaliyoathirika na shambulio la karibuni ni pamoja na Irbin,Duma na Muadhamiya.

Angalia picha zaidi hapa chini

The activists said at least 213 people, including women and children, were killedy in a nerve gas attack by President Bashar al-Assad's forces

A man, affected by what activists say is nerve gas, is treated in the Damascus suburbs of Jesreen

Innocent: The dead bodies of Syrian children after an alleged poisonous gas attack fired by regime forces

Bodies of people, including children, activists say were killed by nerve gas

Many women and children were among the dead. The area reportedly bombed is residential

Fighting in Syria has killed an estimated 100,000 people so far

Activists say most of those killed were in their homes

Heartbreak: Relatives and activists inspect the bodies of the dead

Chanzo - BBC Swahili

Picha - Reuters, AP

Soma habari inayofanana na hii hapa chini

Post a Comment

 
Top