Menu
 


Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Dar es salaam Young Africans kinaendelea vyema na maandalizi ya msimu ujao wa ligi uliopangwa kuanza August 24 katika viwanja saba vya miji tofauti.


Kikosi cha mabingwa hao kimekua kikifanya kazoezi katika uwanja wa Bora kijitonyama, jijini Dar es salaam huku kila mmoja akiamini msimu ujao mambo yataendelea kuwa mazuri katika mpango wa kutetea taji lao la ligi.


Kocha msaidizi wa Dar es salaam Young Africans Fred Felix Minziro amesema sehemu kubwa ya kuwajenga kisaikolojia wachezaji chipukizi waliosajiliwa klabuni hapo wameshaimaliza sasa wameingia katika maandalizi ya kikosi kizima kwa ujumla kabla ya mchezo wa kirafiki ambao utakutanisha dhidi ya Mtibwa sugar na kasha watageukia katika mtanange wa kuwani ngao ya jamii dhidi ya waoka mikate Azam FC.Nae beki chipukizi wa Yanga Juma Abdul Jaffer Mnyamani amesema kuwa maandalizi wanayoendelea kuyafanya yanatosha kuwapa ushindi kwenye mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Mtibwa utakaochezwa mwishoni mwa juma hili.Yanga na Mtibwa watashuka dimbani jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top