Menu
 

Winga mahiri wa kimataifa wa Ufaransa, Franck Ribery amedai kuwa na imani ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka duniani maarufu kama Ballon d’Or.


Ribery mwenye umri wa miaka 30 alitajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka Ulaya baada ya klabu yake ya Bayern Munich kutawadhwa mabingwa wa Supercup kwa kuifunga Chelsea kwa changamoto ya mikwaju ya penati.


Pamoja na mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi kumiliki tuzo ya Ballon d’Or kwa miaka minne mfululizo, Ribery anaamini safari hii yuko katika nafasi nzuri ya kumpoka tuzo hiyo Messi.


Ribery amesema msimu uliopita alifanya kila aliloweza ndani na nje ya uwanja akitumia weledi wake wote ndio anajiamini safari hii anaweza kuikwaa tuzo hiyo ya juu kabisa katika soka duniani.


Winga huyo anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa ambacho kinakabiliwa na mechi za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Georgia na Belarus.

Post a Comment

 
Top