Menu
 

Siku moja baada ya uongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans kudaiwa kumuajiri katibu mkuu mpya badala ya Lawrence Mwalusako, kamati ya wazee wa klabu hiyo wameibuka na kudai hawamtambui katibu huyo ambae ni raia kutoka nchini Kenya.Katibu wa kamati ya wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali amesema kama ni kweli viongozi wa ngazi za juu wameamua kufanya maamuzi ya kumuajiri katibu huyo anaejulikana kwa jina la Patrick Nagi wanatakia kutambua wamekiuka kanuni na taratibu zilizoainishwa kwenye katiba inayowaongoza.Uongozi wa klabu ya Simba umeendelea kutoa tahadhari kwa wafanyabiashara nchini wanaoendelea kukiuka taratibu za kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo inayotambulika kisheria.Mwenyekiti wa baraza la wadhamini la klabu ya Simba Khamisi Kilomoni kwa muda mrefu wamekua wakitoa tahadhari hiyo kwa wafanyabiashara wakubwa na wale wadogo lakini imeonekana wanadharaulika, hivyo kwa sasa wameamua kutumia nguvu za kisheria kwa lengo la kukomesha biashara hiyo haramu.Naye Insepekta wa Jeshi la Polisi Mohamed Manyae amesema baada ya kufuatwa na uongozi wa klabu ya Simba na kulalamikia juu ya biashara inayoendelea kufanywa na wafanyabiashara nchini ya bidhaa za klabu hiyo, wameamua kuwa bega kwa bega na uongozi huo kwa lengo la kumaliza tatizo hilo.

Post a Comment

 
Top