Menu
 


Mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi amekiri kuwa ndoto zake ni kuiongoza nchi hiyo kushinda michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil mwakani.
 
Argentina waliibamiza Paraguay mabao 5-2 jana na kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano hiyo mwakani na Messi anataka kufuata nyayo za Diego Maradona ambaye aliiongoza Argentina kushinda taji lake la kwanza la dunia mwaka 1986.
 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Messi amesema kuwa ana ndoto za kushinda Kombe la Dunia watu wote wanataka hivyo Argentina lakini bado safari ni ndefu kufikia mafanikio hayo.
 
Messi aliendelea kusema kuwa Paraguay ni timu ngumu lakini kitu cha msingi wamepata matokeo waliokuwa wakihitaji na kufuzu michuano hiyo haraka.

Post a Comment

 
Top