Menu
 

Mashabiki wa soka nchini wametakiwa kuwa nyuma ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambayo inakabiliwa na mchezo wa mwisho wa kuwani nafasi ya kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya timu ya taifa ya Gambia mwishoni mwa juma hili.

Rai hiyo kwa mashabiki wa soka, imetolewa na katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Angetille Osiah ambapo amesema kuna haja kwa watanzania kuendelea kuwa nyuma ya Taifa Stars licha ya kukosa nafasi ya kufuzu kucheza fainali hizo ambazo zitaunguruma mwakani nchini Brazil.

Amesema mchezo dhidi ya Gambia una umuhimu mkubwa kama alivyosema kocha mkuu wa Taifa Stars Jan Poulsen wakati akizungumza na waandishi wa habari hapo jana.

Wakati huo huo timu ya taifa ya Tanzania imeondoka hii leo kuelekea mjini Banjul nchini Gambia tayari kwa mchezo dhidi ya wenyeji wao ambao umepangwa kufanyika Septemba 07.

Kikosi kilichoondoka kinamjumuisha nahodha na mlindamlango wa Taifa Stars Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa, Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent Barnabas.

Post a Comment

 
Top