Menu
 Uongozi wa klabu Mbeya city umetangaza hali ya kikosi chao kuenedeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Dar es salaam Young Africans kama walivyofanya wakati wa mchezo wao wa pili dhidi ya maafande kutoka mkoani Pwani ruvu Shooting.Mwenyekiti wa klabu hiyo inayocheza ligi kuu kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwake Mussa Mapunda amesema kikosi chao kipo tayari kupamabna na mabingwa hao kwa hali yoyote ile na kuhakikisha kimaliza dakika 90 kwa kuibuka na ushindi.Nae kocha mkuu wa Mbeya City Juma Mwambusi amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kesho ambao ana hakika utakua mgumu kutokana na uimara wa wapinzani wao.

Mchezo huo umepangwa kuchezeshwa na muamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani huku akitajwa kuwa ni James Mhagama kutoka mjini Songea mkoani Ruvuma.Wakati Mbeya City wakiwakaribisha Dar es salaam Young Africans katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sokoine huko jijini Mbeya wekundu wa MSimbazi kesho watacheza kwa mara ya kwanz akatika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam baada ya kuanzia ugenini katika viwanja vya Ally Hassan mwinyi huko mkoani Tabora pamoja na kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.Simba watwakaribisha Mtibwa Sukari katika mchezo wa kesho huku wakiwa na kumbu kumbu ya kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri walioupata katiak mchezo uliopita dhidi ya JKT Oljoro huku wakata miwa kutoka Manungu Turiani mkoani Morogoro nao watakua wakichagizwa na ushidni kama huo walioupata mbele ya ndugu zao Kagera Sugar.Afisa habari wa klabu ay Simba Ezekiel Kamwaga amesema maandalizi ya kikosi chao kuelekea katika mchezo wa kesho yamaeshakamilika hivyo amewataka mashabiki kujitokeza katika uwanja wa taifa kuishuhudia samba ikicheza kwa mara ya kwanza katika uwanja huo tangu msimu huu ulipoanza.Viingilio katika mchezo huo utakaochezeshwa na muamuzi Dominic Nyamisana kutoka mkoani Dodoma vitakuwa sh. 5,000 viti vya bluu na kijani, sh. 8,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000.Pia Azam TV itautumia mchezo huo kwa ajili ya mazoezi (broadcast training) kwa wafanyakazi wake. Hivyo mechi hiyo haitarekodiwa au kuoneshwa moja kwa moja.Michezo mingine ya ligi kuu ya soka tanzani bara itakayochezwa kesho ni kati ya Coastal Union ambao wanarejea nyumbani katika uwanja wa Mkwakwani baada ya kuwalazimisha sare ya bao moja kwa moja Dar es salaam  Young Africans katika mchezo uliopita, kwa kucheza dhidi ya maafande wa jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya Tanzania Prisons.Kuelekea katika mchezo huo kocha mkuu wa Costal union Hemed Moroko amelitupia lawama shirikisho la soka nchini TFF kwa kushindwa kupanga mikakati mizuri ya kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa na mwenendo mzuri wa kuwatumia wachezaji wake ipasavyo.Maafande wa Ruvu Shooting Ruvu Shooting kesho watakua katika uwanja wao wa Mabatini uliopo maeneo ya Mlandizi mkoani Pwani wakiwakaribisha maafande wenzao kutoka wilaya ya handeni mkoani Tanga Mgambo Shooting.Afisa habari wa Rucvu Shooting Masau Bwire amesema katika mchezo huo kikosi chao hakitokuwa tayari kurejea makosa ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, hivyo kimefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuhakikisha kinapata point tatu muhimu.
 
Huko jijini Aerusha katika uwanja wa kumbu kumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid wenyeji wa uwanja huo Oljoro JKT watacheza kwa mara nyingine nyumbani kwa kuwakabili Rhino Rangers kutoka mkoani Tabora.Katika uwanja wa Kaitba mkoani Kagera, waoka mikate jijini Dar es salaam Azam FC wataendelea kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi mbele ya wapinzani wao Kagera Sugar ambao bado hawajaionja tamu ya ushindi tangu msimu huu uliopoanza zaidi ya matokeo ya sare.Nao Ashanti United watakua nyumbani jijini Dar es salaam wakicheza dhdii ya maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Azam Complex.

Post a Comment

 
Top