Menu
 


Majina ya mameneja Roberto Di Matteo , Tony Pulis , Gus Poyet , Alex McLeish pamoja na  Steve McClaren yamekua yakitajwa katika mchakato wa kumsaka mrithi wa meneja kutoka nchini Italia Paolo Di Canio ambae amefungashiwa virago huko Stadium of Light yalipo makao makuu ya klabu ya Sunderland.

Vyombo vya habari nchini Uingereza tangu mapema hii leo vimekua vikiyataja majina ya mameneja hao ambao wanaijua vyema ligi ya nchini humo kwa kusema huenda mmoja wao akapewa ajira na uongozi wa klabu ya Sunderland.

Taarifa hizo zimedai kwamba mameneja wote hao wamekua katika harakati za kutafuta kazi kwa muda wa miezi kadhaa sasa na wapo tayari kuichukua nafasi ya Paolo Di Canio ambae ameionja shubiri ya kutimulia kazi baada ya kushindwa kuanza vyema msimu wa ligi nchini Uingereza.

Hata hivyo katika mlolongo wa mameneja hao Roberto Di Matteo, ambae aliiwezesha klabu ya Chelsea kuandika historia ya kuwa wafalme wa soka mwaka 2012 barani Ulaya, anaonekana kuwa chaguo la kwanza la viongozi wa klabu ya Sunderland ambao bado wanaendelea kujadiliana namna ya kuiziba nafasi ya meneja klabuni hapo.

Paolo Di Canio ambae alipewa ajira huko Stadium of Light mnamo March 31 mwaka huu alifanikiwa kuinusuru klabu ya Sunderland kushuka daraja msimu uliopita baada ya kuikuta ikiwa katika hali mbaya ambayo ilisababishwa na utendaji mbovu wa meneja aliemtangulia Steve Bruce.

Tangu alipoingia klabuni Paolo Di Canio mwenye umri wa miaka 45, alifanikiwa kushinda michezo mitatu pekee kati ya michezo 13 ambayo imeshuhudiwa ikichezwa akiwa kama mkuu wa benchi la ufundi.

Akizungumza mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya West Bromwich Albion ambao ulikua mchezo wa mwisho kwake kama meneja wa klabu ya Sunderland Paolo Di Canio alikiri kikosi chake bado kilikua na matatizo ya kuelewana baina ya mchezaji na mchezaji hivyo ilikua ni vigumu kwake kuanza vyema msimu huu huku wakiwa tayari wameshacheza michezo mitano.

Pia Paolo Di Canio akajitabiria mabaya wakati alipokua akizungumza na vyombo vya habari kwa kusema yeye alistahili kuwajibishwa kwa kosa hilo.


Katika mchezo huo kikosi cha Sunderland kilikubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri, na kabla ya hapo walikubali kufungwa na Arsenal mabao matatu kwa moja huku Cryastal palace wakitanguli

Post a Comment

 
Top