Menu
 Siku moja baada ya baba mzazi wa kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Mustafa Ozil kujitokeza hadharani na kumtetea mwanawe juu ya kashfa iliyotangazwa na raisi wa klabu ay Real Madrid Florentino Perez Rodriguez, hii leo mchezaji huyoa meibuka na kudai yeye si mwenye tabia za kupenda wanawake kama ilivyoelezwa.


Mesut Mustafa Ozil ambae aliihama klabu ya Real Madrid na kujiunga na klabu ay Arsenal siku ya mwisho ya usajili kwa ada ya uhamisho wa paund million 42, amesema yaliyosemnwa dhidi tyake na kiongozi mkubwa wa The Galacticos hayana ukweli wowote na katu hayatomuumiza katika maisha yake mapaya ya kucheza soka.


Amesema yeye binafsi alifanya maamuzi ya kuondoka nchini huispania baada ya kuona viongozi wa klabu ay Real Madrid wapo tayari kumuuza katika klabu ay Arsenal na katu hakuwahi kuwa na tabia chafu kama alizopakaziwa.


Ozil amesema likua na maisha yake binafsi alipoishi katika jiji la Madrid na alitambua ana haki ya kuishi anavyotaka huku akitunza heshima aliyokuwa nayo kutokana na uwezo wa kucheza soka anapokua uwanjani pamoja na kutunza heshima na klabu kubwa aliyokua akiitumikia.


Katika hatua nyingine meneja wa klabu ay Arsenasl Arsene Wenger amesema yanayozungumzwa juu ya mchezaji huyo hayapi nafasi katika utebndaji wake wa kazi zaidi ya kuamini Mesut Mustafa Ozil ni mcheza mwenye kipaji ambacho ana hakika kitamuwezesha kutimika mipango aliyojiwekea.


Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ufaransa amezungumzia hali ya kushangazwa na mipango ya usajili wa Mesut Ozil ilivyokwenda na mwisho mipango hiyo mambo yakaenda vyema kama alivtyokua anatarajia.


Amesema anahakika usajili wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, ulichagizwana usajili wa Gareth Bale ambao uliwagharimu Real Madrid kiasi kikubwa cha pesa ambazo zililipwa kwenye klabu ay Spurs pamoja na usajili wa wachezaji wengine ambao walisajiliwa klabuni hapo siku za nyuma.


Wenger amesema pamoja na kutambua hivyo, bado yeye mwenyewe alishangazwa na hatua ya kusajiliwa kwa Mesut Ozil ambae hapo aawali alikua akitaka kumsajili kwa njia ya mkopo.
Mesut Mustafa Ozil anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal ambacho kitacheza mchezo wan ne katika ligi ya nchini Uinghereza hapo kesho kwa kupambana na Sunderlandf ambao watakua nyumbani huko Stadium of Light.

Post a Comment

 
Top