Menu
 
 Na Shaban Kondo
Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, Leodegar Tenga ameishukuru Kamati ya ligi kwa usimamizi mzuri tangu ilipokabidhi jukumu la kuisimamia ligi kuu katika mzunguko wa pili msimu uliopita.

Raisi Tenga amesema TFF iliamua kuanzisha Kamati hiyo kwa lengo la kutaka klabu zijisimamie zenyewe ili kuongeza ufanisi, jambo ambalo limeleta mabadiliko na kuondoka matatizo katika kuwalipa waamuzi na makamisha wanaosimamia michezo ya ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza.

Katika hatua nyingine rais Tenga amesema kamati hiyo pia imefanikiwa kutekeleza wajibu wa kudumisha utulivu na utawala bora na hivyo kusababisha kasi ya makampuni kutaka kuwekeza katika ligi kuu kuendelea kupewa nafasi kubwa.

Pia amesema kuanzia msimu ujao 2014/2015 klabu za Ligi Kuu hazitaruhusiwa kusajili wachezaji hadi zitakapowasilisha TFF ripoti zao za mapato na matumizi zilizokaguliwa (Audited accounts), hivyo klabu husika zijiandae kwa ripoti hizo za Januari hadi Desemba 2013.

Wakati huo huo, Rais Tenga amesema bado suala la tiketi za elektroniki linafanyiwa kazi na benki ya CRDB ambayo ndiyo iliyoshinda tenda hiyo na liko katika hatua nzuri, kwani nia ya TFF na benki hiyo kuona kuwa linaanza haraka iwezekanavyo.

Post a Comment

 
Top