Menu
 Mwanariadha anaetamba kwa wa mbio fupi duniani, Usain St Leo Bolt amesema huenda akashiriki michuano ya mbio za mita 200 pekee endapo ataamua kuwa miongoni mwa wanariadha watakaoelekea nchini Scotland kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka 2014.

Usain Bolt ambaye ni raia kutoka nchini Jamaica amesema maamuzi ya kushieriki michuano hiyo ambayo itafanyika kwenye jiji la Glasgow yatachangiwa na majadiliano aliyopanga kuyafanya na kocha wake Glen Mills kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Bolt mwenye umri wa miaka 27 amesema michuano hiyo ipo kwenye mipango yake na angependa kushiriki lakini hawezi lakini hawezi kufanya hivyo mpaka atakaposhauriana na kocha wake ambae anamuheshimu kwa kufuata anachomuelekeza.

Hata hivyo mwanariadha huyo amesema hata kama itatokea atakwenda kushiriki michuano ya Jumuia ya Madola bado angependa kushiriki katika mbio za mitya 200 kutokana na kuipenda mbio hizo zaidi.

Usain St Leo Bolt alifanikiwa kunyakuwa medali tatu za dhahabu katika mbio za mita 100, 200 na mita 400 za kupokezana vijiti katika michuano ya olimpiki iliyofanyika mjini Beijing nchini China mwaka 2008 na kurudia tena katika michuano hiyo iliyofanyika jijini London nchini Uingereza mwaka 2012.

Post a Comment

 
Top