Menu
 


Imetumwa na Shaban Kondo.
Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF limetangaza miji itakayotumika kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2015 itakayofanyika nchini Morocco.


CAF ilithibitisha kuwa miji ya Rabat, Marrakech, Agadir na Tangier ndio iliyowasilishwa na kamati ya maandalizi ya michuano hiyo wakati wa kikao chao kilichofanyika jijini Cairo, Misri wiki iliyopita.


Mji mwingine mkubwa nchini humo Casablanca utafanywa kama mji wa akiba kwa ajili ya michuano hiyo ambayo itaanza kutimua vumbi Januari 17 hadi Februari 7 mwaka 2015.


Kwa mara ya kwanza Morocco kuandaa michuano hiyo ilikuwa mwaka 1998 ambapo Cameroon waliibuka mabingwa baada ya kuwalaza Nigeria kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali.


Mbali na michuano hiyo Morocco pia itaandaa michuano ya klabu bingwa ya Dunia itakayofanyika Desemba mwaka huu kwenye miji ya Marrakech na Agadir.


Post a Comment

 
Top