Menu
 


Shirikisho la soka nchini TFF limejitetea kufutia kitendo cha muamuzi alichezeshwa mchezo wa Simba na Mgambo Shooting Stars kushindwa kumzawadia mpira mshambuliaji Khamis Tabwe kama ishara ya kumbu kumbu baada ya kupachika mabao manne katika mchezo huo.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema muamuzi huyo hakufanya makosa kwa kushindwa kumzawadia mshambuliaji huyo kutoka nchini Burundi mpira, hivyo amewataka mashabiki kutambua hatua ya mchezaji kukabidhiwa mpira kama ishara ya heshima mara baada ya kufunga mabao matatu ama zaidi katika mchezo mmoja haipo kwenye kanuni na sheria za TFF ama FIFA.

Hata hivyo Boniface Wambura amesema bado TFF wanatambua umuhimu wa Khamis Tambwe kukabidhiwa mpira huo kaka ishara ya Fair Play na hivyo wanajipanga kufanya hivyo katika siku ambayo hakuitaja.

Hata hivyo kitendo cha Khamis Tambwe kunyimwa mpira mara baada ya mchezo dhidi ya Mgambo siku ya jumatano, kimewauma sana viongozi wa klabu ya Simba ambao walikuwepo kwenye uwanja wa taifa siku hiyo.

Afisa habari wa klabu ya Simba Ezekiel Kamwaga amesema kitendo hicho kimeufedhehesha mchezo wa soka la bongo hasa ikizingatiwa mchezaji alistahili kupewa heshima hiyo anatokea nje ya nchi.

Post a Comment

 
Top