Menu
 

Majuzi tu mtandao huu uliripoti story ya Mesut Ozil na mpenzi wake ambaye ni mwimbaji wa muziki aina ya Pop toka Ujerumani Mandy Capristo na jinsi wawili hao walivyopanga kuliteka jiji la London .

Jarida moja nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliyopita liliripoti taarifa ya kuwepo kwa uhusiano wa siri baina ya star huyo wa soka la Ujerumani Mesut Ozil na star wa masuala ya mitindo na urembo ambaye amewahi kushiriki Miss World akiwa Mrembo namba moja nchini Venezuela Aida Yespica.

Inasemekana kuwa mrembo huyo toka Venezuela ndio sababu kubwa ya Real Madrid kuamua kumuuza Ozil kwa kile ambacho Gazeti La El Mundo limeripoti kuwa mrembo huyo alikuwa “AKIMCHOSHA” Ozil na kumfanya azorote kiuwezo awapo mazoezini na uwanjani.

Gazeti hilo la kila siku katika chapisho lake la siku ya jumapili liliandika kuwa Ozil alikuwa akitumia gharama za Euro 15,000 kukodi ndege binafsi kumfuata mrembo huyo jijini Milan na Jijini Paris ambako yalikuwa makazi yake makubwa pamoja na wakati mwingine kumsafirisha hadi jijini Madrid alikokuwa Ozil ili mradi tu wale naye bata na kupeana raha ambazo zinadaiwa kumchosha Star huyo wa Kijerumani (Ozil).

Taarifa hizo zimepewa uzito na rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye amemuita Ozil mchezaji asiye muadilifu kwa kipaji chake kwani alikosa weledi (professionalism) kiasi cha kuruhusu kiwango chake kupungua kwa sababu ya mwanamke .

Kufichuliwa kwa uhusiano huu wa siri kwa vyovyote kutakuwa na athari kwenye uhusiano wa Ozil na mpenzi wake wa siku zote Mandy Capristo japo mrembo huyo wa kijerumani bado hajatoa tamko lolote kufuatia kuibuka kwa tetesi hizo .

Post a Comment

 
Top