Menu
 


Mwanariadha nyota wa mbio fupi, Usain Bolt wa Jamaica anaamini kuwa mshambuliaji nyota wa klabu ya Real Madrid ndiye mchezaji mwenye kasi zaidi duniani lakini bingwa huyo anayeshikilia rekodi ya dunia kwenye mbio za mita 100 amesema anaweza kumfanya Bale kuwa na kasi zaidi.

Bale alikimbia kwa kasi mpaka kufikia kilometa 40 kwa saa wakati wa mchezo baina ya Madrid na Villarreal akiwa nyuma kidogo ya kasi aliyotumia Bolt wakati anaweka rekodi ya dunia.

Bolt ambaye anashikilia ubingwa wa olimpiki na dunia katika mbio za mita 100 na 200 amesema anaweza kumfundisha Bale kukimbia kwa kasi zaidi kama mchezaji huyo na Madrid watamuhitaji.

Bolt aliongeza kuwa amewahi kufanya mazoezi na Cristiano Ronaldo na yuko tayari kufanya hivyo na nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspurs.

Post a Comment

 
Top