Menu
 


Vikosi vya usalama vinaendelea na juhudi za kukabiliana na magaidi walioteka nyara baadhi ya wakenya katika jengo la Westgate
 
14:56 Mkuu wa majeshi Meja Jenerali Julius Karangi amesema magaidi hao wanaweza kujisalimisha ikiwa wanataka kwa sababu jeshi litakabiliana nao vilivyo. Pia amesema kuwa Kenya inakabiliana na magaidi wa kimataifa

14:35 Ole Lenku anasema kuwa hali ingali tete lakini vikosi vya usalama vya Kenya vinakaribia kuwazingira magaidi hao...

14:30 Ole Lenku anasema kuwa wanajeshi kumi wamejeruhiwa na wanapokea matibabu. Pia mateka karibu wote wameweza kuokolewa. Ole Lenku pia amesema kuwa wameweza kuwaua magaidi wawili

14:28 Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku anasema kuwa moshi ulitokana na moto uliosababishwa na magaidi wlaioko ndani ya jengo hilo kujaribu kusambaratisha juhudi za wanajeshi wa Kenya dhidi yao

14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti jengo hilo lote na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka
14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

13:54: Mwandishi wa BBCIdriss Situmaaliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo.

13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao

3:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha
13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab
12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa


Raisi wa Kenya uhuru kenyata amewaomba wakenya kuwa watulivu wakati Huu   ambapo vikosi vya usalama vinafanya jitihada kuhakikisha watu waliobaki kaitka jengo la WEST GATE wanaokolewa huku akisisitiza kuwa serikli yake itapambana na magaidi popote pale walipo.
 
Rais Kenyatta ametoa kauli hiyo  wakati akihutubia taifa jana  juu ya tukio la kuuwawa kwa watu wapatao 68 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa,ambapo alitoa hotuba hiyo  mbele ya ya viongozi mbalimbali  wa kisiasa akiwemo aliekuwa waziri mkuu wan chi hiyo  raila odinga. 
 
 Aidha rais uhuru kenyatta amesema vita hii  haihusu dini yoyote wala kabila lolote bali ni vita ya ugaidi.
 
Tukio hilo limetokea tangu jumamosi sept 21 ambapo mpaka sasa bado kuna watu wameshikiliwa na wavamizi hao ndani ya jengo hilo la WEST GATE MALL lakini serikali ya kenya imewahakikishia wananchi kuwa inafanya jitihada zote kuwaokoa watu walioko ndani ya jengo hilo.
 
Askari wa Kenya wakiwa katika harakati za uokoaji

Post a Comment

 
Top