Menu
 


Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania Profesa Sospeter Muhongo, ametangaza rasmi kuliunda na kulisuka upya Shirika la Ugavi wa umeme nchini TANESCO ili lidanye kazi kwa ufanisi mkubwa.

Waziri Muhongo, ametoa kauli hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari mkoa wa Mbeya muda mfupi kabla ya kuanza ziara yake ya kukagua na kuzindua miradi ya umeme mkoani hapa.

Amesema serikali inalazimika kuunda upya uongozi wa TANESCO kutokana na shirika hilo kutokuwa na matokeo makubwa tangu kupatikana kwa uhuru.

Aidha amesema serikali inaendelea na adhama yake ya kuendelea na uzalishaji katika mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira.
MSIKILIZE HAPA Waziri MUHONGO.

Post a Comment

 
Top