Menu
 

Rapper ONE INCREDIBLE ameamua kufyatua Nakala nyingine za Albamu ya SOGA ZA MZAWA aliyoizundua mwaka jana na kumfanya kuahirisha kutoa Albamu yake mpya ya RAP(Representing Africa Popote), iliyotakiwa kutoka rasmi November 16 na hivyo kumfanya aisogeze mbele hadi Mwezi Juni mwakani baada ya kutengeneza menejimenti mpya.


 Akipiga Stori na Kipengele cha Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha Redio Bomba FM 104.0MHz Mbeya Hitmaker huyo wa The Incredible, Rap Science One Incredible hapa anafunguka. "Nilikuwa nimeacha kufyatua nakala kwa sasa hivi, lakini kuanzia Jumamosi zitaanza kupatikana tena, kwa kifupi ni kwamba Albamu niliacha kuziprint kama miezi miwili na nusu iliyopita, kutokana na suala la kwamba nilikuwa najaribu kuestablish Menejimenti yangu mwenyewe na vilevile kwa sababu nilikuwa nimetoka lebel na kumaliza contract kwa hiyo nilikuwa na suala jipya la kuweka menejimenti mpya na jinsi ya kudistribute kazi zangu kwa hiyo nilikuwa nimestop"... 


Hakuishia hapo. "Lakini kuanzia Jumamosi ijayo kwenye ile HIP HOP Matching lines nitaanza tena kuziachia Albamu kama kawaida lakini Albamu yangu ya RAP itatokwa mwakani mwezi wa 6. Kwa hiyo Tarehe 2 vilevile watu wategemee kuna ngoma mpya nitaachia, ni Albamu niliyoizindua mwaka jana SOGA ZA MZAWA, kwa sababu watu wengi walikuwa wamedemand lakini nilikuwa nimeacha kuzisambaza kwa sababu vilevile nilikuwa kuhandle na mambo mengine na menejimenti nilikuwa nataka kuweka mpya kwa hiyo ni mambo ambayo yalikuwa yemenikeep busy kwa stahili hiyo".

Bofya hapa Kumsikiliza zaidi..

Post a Comment

 
Top