Menu
 


Hitmaker wa Jikubali BEN POL a.k.a BEN PIZEEH amesema kutokana kazi nyingi za Video Directors huchangia kwa asilimia kubwa kukosa ubunifu kwenye uandishi wa Script na kuwepo na wimbi la mfanano wa video na ili kuepukana na adha hiyo kwa sasa ameamua kuchukua jukumu la kujiandikia Script za video zake na kuwashirikisha jamaa zake.

Akipiga Stori na Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha Bomba FM 104.0MHz Mbeya na hapa BEN POL anaelezea "Niko kwenye maandalizi ya Video ya WA UBANI, pengine katikati ya November Mungu akijalia tunaweza tukawa tumefikia mahali, nategemea kuitoa before Desemba kwa hiyo bado na discuss kwa sababu sasa hivi tunatengeneza Script ili tujue itamfaa Director gani, kwa sababu naepuka pia kumpa Director atengeneze Script kwa sababu ya kuepusha kufanana video, kwa hiyo Script nimetafuta watu ambao wanauwezo wa kuandika Script nimewapa wimbo ndio tunapokea sasa hizo script kwa ajili ya kuzilinganisha ili apewe Director ambaye anayeweza kwenda na hiyo Script".

BEN POLameendelea kutoa ufafanuzi kwa kutolewa mfano wa video yake JIKUBALI aliyofanya na Director NISHER  "Kwa sababu ukiangalia video yangu ya JIKUBALI kidogo ina utofauti, ina Uniqueness, kwanza ni mzigo niko pekee yangu video yote na bado haikuboi machoni kuiangalia, location ilivyotumika, action  zilivyokuwemo mule  ndo hayo mambo ya mtu unakijadili kitu mwenyewe, wewe na timu yako kwamba ok nataka video yetu iwe hivi  kwa hiyo tunampa Director kama Director anakitu cha kuongezea katika mawazo yetu ni sawa, lakini sio  tumpe Director  halafu kazi ya kushuti na kazi ya kuandika Script kichwa chake kimoja anatoa kazi 10,  anapata kazi ya wasanii 10 tofauti katika hao kumi hata sita lazima watafanana video kwa hiyo kulikuwa na attendance katikati video zinafanana sana  umeona? kwa hiyo ndo hicho  kitu ambacho pia mimi nilikuwa nimekiepuka na kujaribu kukikwepa, ndio maana nimekuja na wazo la kutengeneza script yangu mwenyewe".

Aidha alipoulizwa Je, Video zinakidhi viwango vya ushindani ukilinganisha na gharama za malipo ya kushuti video? BEN POL alikuwa na haya ya kujibu. "Unajua mimi napenda kuheshimu  standard ambazo mtu amejiwekea nikienda sehemu nataka kununua kitu mtu akisema anauza milioni kumi na akakomaa kwa milioni kumi hiyo hiyo, yeye ameamua kujiwekea hiyo  standard yake hiyo unamlipa hivyo hivyo anavyotaka.. kwa mfano mimi wimbo wa JIKUBALI, JIKUBALI audio  nimetumia karibia Milioni moja kurekodi audio tu ushafahamu! Wakati milioni moja nilikuwa na uwezo wa kurekodi nyimbo nne katika studio zingine umeona! kwa hiyo kwa nini niliamua kumlipa mtu karibia milioni  kurekodi JIKUBALI audio yaani kurekodi tu audio kwa sababu unakuta mtu amejiwekea Standard zake umeona! Kwa hiso utaona useme ndio au hapana  na ukisema hapana ni sawa ni biashara, mmeshindwana hamna tatizo ni sawa kabisa kwa hiyo ndio ilivyo kwa hiyo director video akikuambia Five M kushuti au Three M ukiona anastahili na ukiona misimamo yake ni hiyo na wewe unataka kufanya naye kazi inabidi umlipe hata kama unajua kuna sehemu nyingine unaweza kushuti kwa bei nafuu lakini unachoangalia huyo mtu kwanini amehitaji hiyo na hizo standard zake pengine ukimlipa anavyotaka atakufanyia kazi nzuri".

Hata hivyo ameeleza sababu iliyomsukuma na kuamua kufanya Video yake ya JIKUBALI na Director NISHER "Kikubwa niliona ni mtu ambaye ana moto, unajua mtu anapokuwa ameanza halafu ana moto obvious anataka kufanya vitu vizuri vikubwa yaani damu inachemka unaweza kusema anatafuta  exposure  pia kwa hiyo nilimpa kwa sababu hizo, kwa sababu niliona yeye kazi zake za mwanzo alizozifanya za akina MABESTE za akina nani ni kazi kali sana, anafanya kwa nguvu sana  na ubora wa hali ya juu umeona kwa hiyo nikaona huyu mtu akipata audio nzuri anaweza kufanya kitu kikubwa  ndio maana nikafikiria kumpa kwa hiyo nikaona bado ni mpya, bado ana njaa, bado ana ubunifu mwingi,  unajua tofauti na ukimpa Director ambaye ameridhika ana miaka mitano, kumi katika industry anaweza akakufanyia kama moja ya kazi zake za kila siku kwa hiyo mimi nilikuwa naiepuka, kwa hiyo mimi nilikuwa nataka kama mtu unampa kazi afanye kazi hiyo hiyo pekee yake".

Bofya hapa kumsikiliza zaidi BEN POL

Post a Comment

 
Top