Menu
 


Hali ya muandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro aliyejaruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzie inaendelea vizuri lakini bado yupo chini ya uangalizi maalum wa madaktari.

Kwa mujibu wa madaktari waliomfanyia upasuaji wa kuondosha risasi iliyokuwa tumboni Ufoo anahitaji muda mwingi wa kupumzika ili aweze kupata nafuu na kurudi katika hali yake ya kawaidia.Muandishi huyo alipelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili akitokea Hospitali ya Tumbi Kibaha Mkoani Pwani ambapo alipelekwa mara baada ya kukutwa na tukio hilo.

Ufoo alipigwa risasi ya mguuni na tumboni na mzazi mwenziwe maeneo ya Kibamba CCM nyumbani kwa mama yake Anastazia Peter Saro ambaye naye aliuwawa kwa kupigwa risasi na Ansel Mushi mzazi mwenzie na muandishi huyo.
         
 Kwa mujibu wa Kamishna wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam  Suleiman Kova dalili za tukio hilo zinaonyesha kuwa ni masuala ya kifamilia na uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini chanzo chake.

Post a Comment

 
Top