Menu
 


 Benjamini Muhingwa mkazi wa Rujewa mwenye umri wa miaka 48, amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya na kusomewa shtaka la kumbaka na kumsababishia ujauzito mwanae mwenye umri wa miaka 14.

Akisoma shtaka linalomkabili mshtakiwa Benjamini Muhingwa mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya Mbarali Kinabo Minja, mwendesha mashtaka wa Polisi Luchagula Mazoya amesema mshtakiwa alikamatwa Oktoba 18 mwaka huu kwa tuhuma za kumpatia mtoto wake ujauzito wenye miezi mitano sasa.

Aidha mshtakiwa alikana shtaka linalomkabili na amerudishwa rumande, baada ya kukosa mdhamini mwenye mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi Milioni mbili na keshi hito itaanza kusikilizwa Oktoba 28 mwaka huu.

Hata hivyo Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto Sophia Simba amesema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia. 
Bofya hapa kumsikiliza .......

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk Marry Mwanjelwa, akizungumzia suala hilo la unyanyasaji wa kijinsia kushamiri kwa sasa alikuwa na haya ya kusema...

Post a Comment

 
Top