Menu
 

 
Tangu nimeachia video mpya ya wanasubiri nife, nimepata simu nyingi siku ya leo, na wengi wananiuliza kama hii nyimbo nimeandika kwa ajili ya kumdiss Ney wa Mitego na clouds fm? Kutokana na mistari ifuatayo

''najua mnajua kuwa mnajua, ila hamuwezi nichukua kwenye tour, mnawachukua wasiojua. mitego wanayotega naitegua, ingawa wachache wanabana, ninafanya, ninafana na kupiga hatua''

JIBU
Huu wimbo nimeandika mahususi kwa watu wote, ambao wanajifanya hawaoni umuhimu wangu, wakati nafsi zao zinajua fika kuwa mimi ni bora zaidi ya hao ambao wanawafanya waonekane bora ,sikuandika kwa lengo la kumdiss NEY au Clouds fm ila kama mistari Imewagusa na maandiko yangu yametafsirika hivyo ni furaha kubwa sana kwangu, hicho ni kitu ambacho mwandishi yeyote anatamani iwe hivyo,kwa kuwa hadi mnatafsiri maanake mnajadili, endeleeni kujadili ili sanaa yetu ikue..

NB
SHUKRANI KWA WOTE MNAO SHARE NA KUENDELEA KUSHARE VIDEO YANGU HII MPYA facebook,kwenye page zenu, blogs na website zenu au kucheza audio ya huu wimbo, shukrani sana kwa BONGO5 kwa uchambuzi wenu maana ndio umepelekea watu wengi kunipigia simu,nina hakika watu wote wangekuwa wanafuatilia kama nyinyi hii sanaa ingefika mbali sana

MUNGU AWABARIKI WOTE.......

AZMA/THE AFRICAN AMBASSODOR/TAMADUNI MUZIK
CHEKI VIDEO YAKE HAPA CHINI

 

Post a Comment

 
Top