Menu
 

Kiungo kutoka nchini Uingereza na klabu ya Arsenal Jack Wilshere ameomba radhi kufutia kitendo cha uvutaji wa sigara hadhari alichokifanya mwishoni mwa juma lililopita na kupelekea kupigwa picha zilizoanikwa katika magazeti.

Jack Wilshere ameomba radhi huku akiutaka umma wa mashabiki wa soka duniani kote kutomuelewa vibaya kufutia kitendo hicho ambacho amesema kilijitokeza kwa bahati mbaya na wala hakukusudia kufanya hivyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema sio tabia yake kuvuta sigara kama alivyoonekana katika picha za kwenye magazeti, hivyo amesisitiza suala al kusamehewa kwa kosa hilo ambalo linamfanya ajionene kama mpuuuzi miongoni mwa wanajamii wanaomtazama kwa jicho jema.

Amesema tayaria meshazungumza na bosi wake Arsene Wenger na amemuelezea kwa kina juu ya suala hilo na mwishiwe walilimaliza kibinaadam kwa kumtaka radhi mzee huyo wa kifaransa ambae anamchukulia kama baba yake mzazi.

Jack Wilshere ambae jana aliifungia timu yake ya Arsenal bao la kusawazisha wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya West Bromwich Albion, alipigwa picha akiwa anavuta sigara nje ya ukumbi wa starehe, saa chache mara baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo Arsenal waliibuka na ushidni wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Societa Sportiva Calcio Napoli, kutoka nchini Italia.

Wakati huo huo meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amempongeza Jack Wilshire kufutia juhudi binafsi ambazo ziliisaidia timu yake kupata point moja ikiwa ugenini baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya West Bromwich Albion hapo jana.

Arsene Wenger amesema amefurahishwa na binafsi za kiungo huyo na kwa hakika anaamini baada ya klufanya mazuri katika mchezo wa jana, bado kuna mengi na mazuri yanakuja kutoka kwake.

Katika mchezo huo Arsenal walikua nyuma kwa muda wa dakika 21 baada ya kiungo kutoka nchini Argentina Claudio Yacob kuifungia West Brom bao la kuongoza katika dakika ya 42.

Post a Comment

 
Top