Menu
 

 Majengo ya shule ya msingi Sabasaba iliyopo Manispaa ya Iringa, ambapo ndipo shughuli ya ugawaji wa msaada wa madawati yaliyotolewa na mbunge Ritha Kabati wa CCM mkoa wa Iringa ilifanyika.
 Mbunge Ritha Kabati (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wakuu wa shule nane ambazo zimenufaika na msaada wake wa madawati, wa kwanza kulia ni ofisa elimu vifaa na takwimu Bi. Jane Mwalongo.
 Bw. Salim Abri "Asas" (mwenye kofia nyeupe na kanzu) akiwa katika picha ya pamoja katika hafla ya kukabidhi madawati kwa shule za msingi 8 za Manispaa ya Iringa.
 "Yaani mh. Kabati!! Utadhani ulijua kuwa Shuleni kwangu kuna tatizo kubwa la madawati, asante sana," Akisema mwalimu huyo. 
 "Ninashukuru sana Mh," Ni mmoja wa walimu wa shule 8 zilizonufaika na msaada huo wa madawati akimshukuru mbunge Ritha Kabati. 
 Afisa elimu vifaa na takwimu Manispaa ya Iringa akitoa orodha ya majina ya wakuu wa shule watakaopatiwa msaada wa madawati, yaliyotolewa na mbunge Ritha kabati.
 Mmoja wa walimu wa shule zilizonufaika na msaada wa madawati akimshukuru mbunge Ritha Kabati.

 Baadhi ya walimu waliofikiwa na msaada wa madawati wakimshukuru mbunge Ritha Kabati, ambaye alikabidhi madawati 100 kwa shule 8 za manispaa ya Iringa.
Mh. Aly Mbata diwani wa Kata ya Kitwiru akitoa shukrani kwa mbunge wa viti maalumu mmkoa wa Iringa Mh. Ritha kabati (mwenye Blauzi nyeusi). 
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Bw. Abeid Kiponza(mwenye koti jeusi) akiwa na Kamanda wa Vijana mkoa wa Iringa Bw. Sali Abri Asas katika hafla ya kukabidhi madawati, vitabu na Komyuta.
Afisa elimu vifaa na takwimu Bi. Jane Mwalongo akitoa taarifa ya madawati na idadi ya wanafunzi katika Manispaa ya Iringa. 
 Mbunge Ritha Kabati akizungumzia mpango wake wa kutoa msaada wa madawati, Vitabu kwa shule 5 za sekondari na Kompyuta.
WAKATI Waislam kote nchini wakisherehekea sikukuu ya Idd El Haji, sikukuu ya kuchinja wanyama wenye miguu minne, Watanzania wameshauriwa kubadili mfumo wa utoaji wa Zawadi na misaada katika sherehe na sikukuu, kwa kujikita kutoa misaada yenye tija kwa jamii, ili kupunguza changamoto zinazoikabili Serikali,  ikiwemo sekta ya  elimu,  na kuacha kuegemea kutoa zawadi na misaada ya vyakula pekee.

Hayo yamezungumzwa na Kamanda wa Vijana CCM mkoa wa Iringa, Bw. Salim Abri Asas, wakati mbunge wa Viti maalumu CCM Mkoa wa Iringa Mh. Ritha Kabati akiitumia sikukuu hiyo ya Idd El  Haji kwa kutoa msaada wa madawati 100 kwa shule za Manispaa ya Iringa zinazokabiliwa na changamoto hiyo, shughuli iliyofanyika katika shule ya Msingi Sabasaba mjini Iringa.

"Kuna haja sasa kwa jamii kuona umuhimu wa kutoa misaada na zawadi katika sikukuu na sherehe mbalimbali kwa kujikita katika jambo la elimu, mfano vitabu, madaftari, madawati na vitu vya muhimu, siyo kutoa misaada na zawadi ya vyakula tu, hata mimi hapa nimejifunza sana jambo hili, huu ni mfano wa kuigwa sana," Alisema Salim Abri.

Aidha amesema endapo jamii itabadilika kwa kufanya matendo ya aina hiyo ya utoaji wa misaada na zawadi zenye tija changamoto mbalimbali zitatatulika, na hivyo sekta ya elimu na nyingine kupinguza kama siyo kumaliza kabisa matatizo yanayowakabiri wananchi.


Akizungumzia sababu za misaada hiyo Mbunge Ritha Kabati amesema ameona ni vyema kutoa msaada unaoishi kwa muda mrefu, badala ya chakula ambacho kingeisha thamani yake baada ya muda mfupi.


Mh. Ritha amesema changamoto ya madawati na vitabu amekuwa akiiona katika shule nyingi, pindi anapoalikwa katika shughuli mbalimbali na hivyo kuona upo umuhimu kuifanyia kazi yenye tija sekta hiyo ya elimu kwa kutatua changamoto za hiyo ya madawati, vitabu kwa shule 5 kati ya 13 anazozifanyia mchakato huo, pamoja na Comyuta, lengo kuu likiwa ni kuleta ufanisi na kuboresha sekta ya elimu.

Martin Yesaya mkuu wa shule ya msingi Ukombozi na Iddy Hamis Khanju mkuu wa shule ya msingi Mlangali wamesema endapo wananchi kwa ujumla watajikita katika kuisaidia sekta hiyo muhimu ya elimu, basi changamoto zingekuwa historia na hivyo wanafunzi wangeza kufundishwa na kujifunza katika mazingira rafiki.

Kwa mfano mimi pale shuleni kwangu Mlangali ninaupungufu wa madawati 285, sasa hili ni tatizo, kwani hata walimu inamuwia vigumu kumfundisha mwanafunzi ambaye amekaa kwa kubanana katika dawati, lakini kupitia msaada wa mbunge huyu kwa namna moja tatizo shuleni kwangu limepungua," Alisema Khanju. 

Ofisa elimu takwimu na vifaa, wa Manispaa ya Iringa Jane Mwalongo amesema Manispaa inaupungufu wa madawati  13429, na hiyo ni kutokana na uwepo wa idadi ya wanafunzi elfu 26, 858, huku mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mlangali Idd Khanju akisema yule yake inakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati 285.

Kwa hisani ya OLIVER MOTTO BLOGU

Post a Comment

 
Top