Menu
 


 

Mgombea nafasi ya uraisi wa shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi hii jana amezindua rasmi kampeni za kuwani nafasi hiyo huku akitoa ahadi ambazo ana hakika atazitekeleza endapo atapewa nafasi  na wajumbe wa mkutano mkuu mwishoni mwa juma hili.


Jamali Malinzi ambae anaiwani nafasi hiyo kwa mara ya pili, baada ya mwaka 2008 kushindwa na raisi anaemaliza muda wake Leodger Chilla Tenga, amesema soka la Tanzania linahitaji msaada mkubwa ili liweze kufikia malengo yake pamoja na kuwafurahisha watanzania ambao wana uchu wa mafanikio.


Malinzi amesema mzizi mkubwa wa maendeleo ya soka nchini unatakia kujikita katika idara ya ufundi ya shirikisho la soka nchini na kama atapata nafasi ya kuwa raisi wa TFF atahakikisha idara hiyo inaboreshwa kwa lengo la kuufufua upya mkakati wa soka kuanzia kwa vijana wenye umri mdogo.

Katika hatua nyingine Jamali Malinzi akaguzia suala la mikataba kwa kusema endapo atapewa fursa ya kuliongoza shirikisho la soka nchini kwa ridhaa ya wapiga kura, atahakikisha kuwa muwazi katika hatua za kuingia mikataba na makampuni ambayo kwa sasa yanatumia kivuli cha soka kujinufaisha binafsi pamoja na baadhi ya watu wasiolitakia mema soka la Tanzania.

Post a Comment

 
Top