Menu
 


Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema haihusiki na utoaji wa kibali cha tiba mbadala kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakifikiria na kwamba  Imetoa ufafanuzi wa kazi zinazofanywa na ofisi hiyo kwa watu wanaojihusisha na tiba za asili.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia kuwepo kwa baadhi ya wataalamu wa tiba asili kutumia jina la Mkemia Mkuu wa serikali kama kibali cha kuuzia dawa zao kwa wananchi kwa kigezo cha kuthibitishwa na Ofisi hiyo.

Meneja wa kanda ya mashariki wa wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali Daniel Ndiyo, amesema kazi inayofanywa na ofisi hiyo kwa wataamu wa tiba mbadala ni kutekeleza maombi ya wateja wao hasa wanapokuwa wanataka kupata uthibitisho kama dawa ina sumu au laa.
SIKILIZA HAPA>..

Post a Comment

 
Top