Menu
 


FIFA-logo-300
Huko mjini Zurich nchini Uswiz:
Shirikisho la soka duniani FIFA limekamilisha mpango wa kupanga michezo ya hatua ya mtoano Ukanda wa Barani Ulaya kabla ya kueelekea katika hatua ya mwisho wa kupanga makundi na ratiba ya fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 mwishoni mwa mwaka huu.

Katika ratiba hiyo ya michezo ya hatua ya mtoano iliyopangwa jana na FIFA inaonyesha timu ya taifa ya Ufaransa imeangukia mikononi mwa timu ngumu ya Ukraine.

Ufaransa ambao walimaliza katika nafasi ya pili baada ya timu ya taifa ya Hispania ambayo ilimaliza kinara wa Kundi la Tisa ukanda wa barani Ulaya itaanzia ugenini na kisha kumalizia nyumbani kabla ya kujua hatma ya kuelekea nchini Brazil mwaka kesho.

Timu ya taifa ya Ukraine nayo ilimaliza katika nafasi ya pili, nyuma ya timu ya taifa ya Uingereza ambayo ilikua kinara wa kundi la nane.

Mchezo mwingine wa hatua ya mtoano ambao utakua na mvuto utamuhusha Cristiano Ronaldo ambae anaitumikia timu ya taifa ya Ureno dhidi ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic *Ibra Cadablra* ambae anaitumikia timu ya taifa ya Sweden.

Michezo mingine ni kati ya ;
Ugiriki v Romania
Iceland v Croatia

Mkondo wa kwanza wa michezo hiyo ya hatua ya mtoano ukanda wa barani Ulaya imepangwa kufanyika Novemba 15 na michezo ya mkondo wa pili itachezwa Novemba 19.

Ifahamike kwamba tayari timu Tisa kutoka ukanda wa barani Ulaya zimeshakata tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014, na sasa zinatafutwa timu nne kwa kutimiza idadi ya nchi 13 kutoka katika bara hilo ambalo lipo chini ya UEFA.

Post a Comment

 
Top