Menu
 


Aliekua meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Man Utd, Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa hana mpango wa kurejea katika kazi ufundishaji.

United kwa sasa wako katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza chini ya kocha mpya David Moyes ambaye alichukua mikoba ya Ferguson mwezi Mei mwaka huu.

Ferguson amesema kuwa hana mpango wakurejea kufundisha tena na kuongeza kuwa United iko katika mikono salama kwa sababu Moyes ni kocha mzuri.

Ferguson mwenye umri wa miaka 71 aliongeza kuwa Roman Abramovich alimuhitaji kwenda kuinoa Chelsea wakati alipoinunua klabu hiyo mwaka 2003.

Kocha huyo amesema Abramovic alitumia wakala kunishawishi kuifundisha Chelsea lakini alikataa ombi hilo.

Post a Comment

 
Top