Menu
 


Hitmaker wa Majanga, Nimevurugwa SNURA MUSHI amekanusha taarifa za kuacha kufanya movie kwa sababu ndio sehemu ambayo ilimfanya yeye ajulikane zaidi kuliko music.

Akipiga stori na Chumba Cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba hapa Bomba FM 104.0MHz amesema kwamba kwa  sasa yeye anajiandaa kutayarisha movie yake mwenyewe ambayo itafahamika kwa jina la majanga ya SNURA.


Katika hatua nyingine amesema  kuwa sababu kubwa ya Tanzania kushindwa kufanya vizuri katika tasnia ya Muziki inasababishwa na Serikali kushindwa kusimamia kazi za wasanii ambapo inapelekea wasaniikupata hasara katika kazi zao.Aidha ameongeza kuwa kuna utofauti mkubwa sana katika maslahi kati ya music na movie ambapo amesema kwenye music kunasababisha  yeye apate shoo nyingi kuliko kwenye movie kwa sasa..

Post a Comment

 
Top