Menu
 Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Selemani Msindi a.k.a AFANDE SELE kutoka Mji Kasoro bahari Morogoro, ameshtumiwa kuwa ndio chanzo cha mvunjiko wa kundi la Watu Pori licha ya kutafutwa mara kwa mara na wasanii wenzake akiwemo Mc Koba kwa nia ya kulirudisha kundi katika gemu.

 Akipiga Stori na Chumba cha Sindano kupitia kipindi cha Kali za Bomba cha Kituo cha redio Bomba FM Mbeya msanii MC Koba anafunguka "Kiukweli hakuna mtu anayependa mvunjiko mimi kama mimi binafsi roho inaniuma sana kwa sababu nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kupigania uwepo wa Kundi la Watupori, lakini kushindikana kwake au ugumu wake unaletwa na Btother tunayempa nafasi, niseme nini tunampa dhamana ya kutuongoza kwa sababu Koba hawezi kuwa kiongozi, Dito hawezi kuwa kiongozi".

MC Koba akimshtumu Afande Sele kuwa ndo chanzo cha mvunjiko "Afande alikuwa anatutupia sisi mzigo unajua, Vijana ndio hawataki, vijana ndio hawataki(kwa msisitizo) sasa mimi nikasema kwamba any way kwa sababu nimesikia rumours  za namna hiyo kutoka kwa watu wengi, hata mimi watu walikuwa wananipigia simu kwanini mnafanya hivyo "unaona bana" muziki unashuka Watu Pori wameshuka na vitu kama hivyo unajua. Kwa hiyo mimi nikaona kwa sababu napenda umoja wetu ngoja basi tufanye track".

Hapa anasema kuwa Albamu katika kundi yeye ndio alikuwa akishiriki kwa asilimia kubwa sana kuliko wenzake, "Kwa sababu gani nasema kuna Asilimia 100 ambazo mimi nime-perform ni kwa sababu Chorus zote za ile Albamu zimefanywa na Koba, tuseme umeelewa. Kwa hiyo najua kabisa katika muziki chorus ni kitu kikubwa katika wimbo wowote chorus ndio kitu kikubwa kinachomtuliza mtu, kinachomread mtu, kinamshika mtu. Kwa hiyo chotus zote zimeandikwa na Koba na zimeibwa na Koba, lakini watu walikuwa hawajui Koba na Dito wanafanana kidogo hivi kwa hiyo Dito alikuwa anamficha Koba kwa sababu ya jina lake.
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA .

Kwa upande wake Hitmaker wa Wapo, Dito hapa anazungumzia kuhusu Watu Pori baada ya kuulizwa kama anafahamu chochote kuhusu kutupiwa lawama na Afande Selle kutokana na kupiga chenga kurudisha kundi katika gemu. "Sidhani unajua Watu Pori, Watu Pori watabaki, Watu pori ni mtu yeyote ambaye yupo katika zile himaya, haya mambo mengine yanayoendelea ni katika kujijenga tu sisi wenyewe umeshanifahamu, lazima Dito awe Dito mwisho wa siku na Afande kama Afande mwisho wa siku ushanifahamu kwa sababu ni watu ambao ni brada tofauti, ushanifahamu aaah mimi sidhani kama kuna tofauti namna tunavyoishi kila siku binafsi mimi, hatufanyi vitu kwa sababu ya urafiki au labda ya udugu au sijui ya nini".

Dito Anaendelea kutoa ufafanuzi "Siku hizi ni biashara soko likihitaji yaani mimi binafsi nikiona soko linahitaji Watu Pori kufanya biashara, biashara imekubali nini kitakachonirudisha nyuma, au koba nini kitakacho mrudisha nyuma au Afande nini kitakacho mrudisha nyuma. Soko la sasa linahitaji Afande Sele atoe nyimbo zake, Koba atoe nyimbo zake basi ndo hiko ndo kikubwa kwa hiyo mimi sidhani kama ikitokea biashara kwamba biashara inalazimisha ufanye kitu fulani kisifanyike hakuna hicho kinachoweza kukwamisha kwa mimi hiyo kwa navyosema sasa hivi tunafanya muziki asa business hatufanyi muziki kwa ajili ya udugu, udugu unakuwepo lakini hauingiliani na masuala yetu ya kibiashra".
BOFYA HAPA KUMSIKILIZA.

Hata hivyo Afande Sele akijibu shtuma za kulivunja kundi la Watu Pori "Kundi sio msingi, kwanza sina hata stori kwani lazima kuwa na kundi mimi sina kundi, Koba nilimchukua kama mtoto yatima, Dito kama mtoto yatima nimewalea nyumbani kwangu basi. Kwa hiyo mimi nilikuwa kama bridge kwa sababu kimoyoni Koba hakuwepo alikuwa kama wale watoto wa mitaani ambao wana matatizo na mimi kawaida yangu ni kuwasaidia vijana. Kwa hiyo nikawachukua kipindi kile nikawatengenezea kundi la Gheto Boys likasambaratika, nikatengeneza Watu Pori likaja kusambaratika sasa hivi kila mtu ana maisha yake sio muda wa kutengeneza makundi, makundi kwa kulipwa hela gani bwana. Kwanza toka zamani nilikuwa sina kundi isipokuwa nilikuwa naishi nao pamja isipokuwa niliwatafutia kitu cha kuwauza  ila wao walishindwa kutulia na kuelewa.

Afande Sele anaendelea kutoa ufafanuzi zaidi toka kunaza kwake muziki anadai hajawahi kuwa katika Kundi na sababu za Dito na Koba kukimbia "Kwa hiyo sina kundi isipokuwa naweza kufanya nyimbo na mtu yeyote ila huwa sina kundi, toka nianze muziki yaaah mimi nimeanza muziki na Mr II a.k.a Sugu, Mimi na Sugu kwani tulikuwa kundi au mimi nilikuwa DeiWaka si nilikuwa nafanya na Sugu nyimbo zote si unakumbuka?(alijaji), Kwa hiyo Koba anatakiwa afanye kazi zake na mimi nafikiria nifanye kazi zangu mwenyewe namshirikisha kwa upendo tu, ila kama waliua kundi la Watu Pori  kipindi kile hakuna namna nyingine ya kurudisha kundi ni kupoteza time tu umeona, yaani kipindi kile ambacho Watu Pori ilikuwa imesimama vizuri ndio kilikuwa kipindi cha kutengeneza hela sasa wao mimi nimeshawatengenezea nimeshatumia gharama kibao kuwajenga, baadae wamejiona wamejua wamekimbia wenyewe hakuna aliyewafukuza".

Hakuishia hapo Afande Sele hapa anamsihi Koba atazame maisha mapya huku akieleza kuwa Dito muziki ulisha mshinda "Sasa inatakiwa naye apiganie maisha kama mwenzake Dito anafanya maisha magumu japo sisikii anafanya muziki wowote wala sijui muziki anaofanya, lakini namwona anaishi yuko mjini anakaa vizuri anatembelea gari japo sijui naye anafanya nini kwa sababu naamini muziki ila Koba anapaswa afikirie afanye nini katika maisha yake afanye shuguli zake au muziki au kitu kingine ili mimi Afande Sele nibaki kama Afande Sele sitaki kundi na sina kundi kwa hiyo hata Koba  alivyotudi nilivyomshirikisha kwenye wimbo Amani na Upendo ule ni wimbo wangu upo kwenye remix ya Mashukuru Mageni au vipi kwa hiyo nikaenda studio akafanya kushiriki nikaona mimi sina chuki nikamwambia ingia lakini sio kwamba tunarudisha kundi cha msingi uwaelimishe madogo kuwa makundi ni kudhihirisha woga".
BOFYA KUMSIKILIZA.

Post a Comment

 
Top