Menu
 Uongozi wa tawi la Mpira pesa umesema upo sambamba na kauli iliyotolewa jana na kocha mkuu wa klabu ya Simba King Abdallah Kibaden Mputa ya kuwashutumu baadhi ya wachezaji kwa madai walitumiwa kwa lengo la kukihujumu kikosi chake ambacho kilikwenda mapumziko kikiwa kimefungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Dar es salaam Young Africans.


Mwenyekiti wa twi la Mpira Pesa Ustadh Masoud amesema kauli iliyotolewa na King Abdallah Kibaden Mputa haina utata hata kidogo kwa upande wao kutokana na uchunguzi walioufanya kabla ya mchezo wa jana ambapo walibaini kuna baadhi ya wanachama wenzao wanatumika kuihujumu timu ya Simba ambayo ilikua inaongoza msimamo wa ligi kabla ya michezo ya mwishoni mwa juma lililopita.


Kocha mkuu wa Simba King Abdallah Kibaden Mputa alilibua sakata hilo mara baada ya mchezo wa jana akiwa mbele ya waandishiw a ahabari ambapo alisema wazi sababu zilizopelekea kikosi chake kuonekana dhaifu wakati wa kipindi cha kwanza na kuelekea kichapo cha mabao matatu kwa sifuri.


Wakati Simba SC kukifukuta kwa watani zao wa Jadi Dar es salaam Young Africans hali si shwari kufuatia baadhi ya wachezaji kushutimiwa na wanachama kwa kuaminika huenda walikuwa na agenda ya siri katika mchezo wa jana.


Mwanachama wa klabu hiyo Sudy Tall amesema kuna ulazima kwa uongozi wa Dar es salaam Young Africans kuangalia kwa kina kinagaubaga kilichosababisha uzembe ambao uliwapa ahuweni Simba na kufanikiwa kusawazisha mabao matatu katika kipindi cha pili.

 

Lakini madai hayo ya Sudy Tall, yakapingwa na katibu wa baraza la wazee Ibrahim Akilimali ambae aliahidi kikosi chao kingeibuka na ushindi wa mabao matatu katika mchezo wa jana kwa vyovyote vile.


Akilimali amesema kilichotokea uwanjani yeye binafsia mekubaliana nacho na pia amewataka wanachama wenzake kusahau yaliyopita na kufikiria yajayo na wala muda huu sio sahihi kwao kuanza kumsaka mchawi.

 

Hata hivyo upande wa kocha mkuu wa kikosi cha Dar es salaam Young Africans Erne Brandt wakati wakizungumza na waandishi  wa habari mara baada ya mchezo huo hapo jana, alikiri wazi wachezaji wake alionyesha nidhamu mbovu walipokua uwanjani baada ya kuongoza mabao matatu kwa sifuri.


Amesema ilionekana dhahiri wachezaji wake waliliridhika na hatua ya kuongoza mabao matatu, halia mbayo ilijidhihirisha wakati wa mapumziko kutokana na nderemo na vifijo vilivyokua vikiendelea katika vyumba vya kubadilishia.

Post a Comment

 
Top